Majeruhi wa  mapingano  kati ya  polisi na  wananchi  mjini Iringa 
Mwanahabari  wa  kituo  cha radio  Overcomers Fm Devota Romanus  akiwa wodi namba  7 katika  Hospitali ya mkoa  wa Iringa baada ya kujeruhiwa mguu  wake  wa  kushoto kwa mawe
Askari  polisi aliyejeruhiwa  akipelekwa  wodini kulazwa
Nguo  za majeruhi ambaye  alijeruhiwa kwa  risasi baada ya  kutaka  kuwachoma moto  wanahabari na polisi  ndani ya nyumba  hiyo
Magari  ya  mfanyabiashara huyo yakiwa  yamevunjwa  vioo kwa mawe
Nyumba ya mfanyabiashara  huyo  ikiwa  imevunjwa na  wananchi
Umati  wa wananchi  wa mji wa Iringa  wakikimbia mabomu ya machozi
NA FRANCIS GODWIN
Zaidi ya  watu 10 wakiwemo  askari wanne na wanahabari  wamejeruhiwa  huku baadhi yao  wakitibiwa na kuruhusiwa na wengine  kulazwa katika  Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya  kuibuka kwa mapigano hayo kati ya polisi na wananchi ,mapigano ambayo  yametokana na imani potofu za wananchi katika kuamini ushirikina.
Wananchi hao zaidi ya 200 walivamia nyumba ya mzee wa kanisa moja la kilokole katika mji  wa Iringa  eneo la Frelimo  jina limehifadhiwa  kwa sababu za kimaadili .
Hata  hivyo    pona ya  wanahabari na polisi  waliokuwa  wamefungiwa ndani ya nyumba  hiyo na kushambuliwa kwa mawe  na kunusurika kuteketezwa kwa moto  wakiwa ndani ya nyumba  hiyo ilionekana  baada ya  askari  polisi  wa FFU   kutumia mbinu  kubwa ya kulazimika kutumia risasi ya moto kumshambulia mguuni mmoja kati ya  watu  wanaodaiwa kutaka  kuongoza  wengine  kuichoma moto nyumba  hiyo iliyokuwa na wahahabari ndani ,polisi  na mchungaji mmoja .
Baadhi ya  wananchi  wamelipongeza  jeshi la polisi mkoa wa Iringa kwa  kuokoa maisha ya  wanahabari hao na  watu wengine zaidi ya 10 ambao  walipaswa  kuuwawa na wananchi  hao .
Wananchi hao  walionekana kuongezeka idadi baada ya  FFU  kuwatisha kwa mabomu ya machozi  huku wakidai kuwa mabomu hayo hayaui na bila polisi  kupata  mbinu ya haraka ya kutumia risasi ya moto   zaidi ya  watu hao  10 wakiwemo  wanahabari  waliokuwa ndani ya nyumba  hiyo  wangekuwa wameuwawa na wananchi hao ambao  waliondoa imani na kikosi hicho  kuwa wamehusika  kuificha misukule  hiyo.
No comments:
Post a Comment