Wadau mbalimbali walikuwepo
HALMASHAURI za Mkoa wa Mbeya, zimetakiwa kutenga maeneo yaliyopimwa kwa ajili ya uwekezaji ili kuepuka migogoro baina ya wananchi na wawekezaji ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro wakati wa ufunguzi wa mkutano wa baraza la biashara la Mkoa wa Mbeya.
Alisema, ni vema halmashauri hizo zikatenga maeneo ya ardhi ambayo tayari wameshayapima kwa ajili ya uwekezaji na si kuwatumbukiza wawekezaji kwenye migogoro na wananchi.
“Halmashauri zinapaswa kuyapima maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya uwekezaji ili kuwaokoa wawekezaji na migogoro ya wananchi ambayo hupoteza muda kwa kupelekana mahakamani,
Alisema, pia halmashauri hizo zinatakiwa kusghulikia matatizo ya wananchi kama vile kulipa fidia kwa wale watakaoitajika kuondoka kwenye maeneo yao kwa ajili ya uwekezaji.
“Halmashauri zinapaswa kufahamu kuwa zinawajibu wa kushughulikia matatizo ya wananchi kama vile kulipa fidia kwa watakaotakiwa kuondoka na si kuwaachia matatizo wawekezaji na ambao huishia kupelekana mahakani,
Aidha, Mkuu huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Balaza hilo aliwataka watendaji wa serikali na wanasiasa kwa ujumla kuacha kupoteza muda kwa kujadili mambo ambayo hayana msingi bali watumie muda huo kujikita kwenye shughuli za maendeleo.
“Tusipoteze muda kuzungumzia mambo ambayo hayana msingi bali tutumie muda huo kuzungumzia mambo ya maendeleo ambayo ndio msingi wa Taifa katika kuleta maendeleo,
|
No comments:
Post a Comment