Wananchi   wa mji mdogo wa Mbalizi, wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya   wakigombania foleni ya kuteka maji, yaliyobebwa kwenye Behewa la treni   inayomilikiwa na Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) siku ya  jana majira ya asubuhi kutokana na uhaba  wa maji unaokabiri mji huo.
Wananchi  waliofika eneo TAZARA huku wengine wakiwa wamepanga  foleni kwa ajili  ya kupata maji ambapo Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) liliteka maji hayo kwa ajili ya  wafanyakazi wake waliopo mji mdogo wa Mbalizi, wilaya ya Mbeya vijijini  Mkoani Mbeya.
 
 Wananchi  waliofika eneo TAZARA huku wengine wakiwa wamepanga  foleni kwa ajili  ya kupata maji ambapo Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) liliteka maji hayo kwa ajili ya  wafanyakazi wake waliopo mji mdogo wa Mbalizi, wilaya ya Mbeya vijijini  Mkoani Mbeya.
*****
 Siku   ya tatu toka hali ya utulivu kurejea mkoani Mbeya, hali imekuwa tete   zaidi katika mji mdogo wa Mbalizi uliopo wilaya ya Mbeya Vijijini ambapo   wananchi wanamtaka Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kuchukua  maamuzi  mazito ya kuwarejeshea mradi wao wa maji ulioporwa na Vigogo wa   Serikali.
Vikosi   kadhaa vya kutuliza Ghasia (FFU) vilionekana jana katika viunga   mbalimbali vya mji huo kwa ajili ya kuwatawanya wananchi baada ya   Serikali kupata taarifa yakuwepo maandalizi ya maandamano ya kudai haki   yao hiyo ambayo walisema Mkuu wa wilaya hiyo Evance Balama alishindwa   kuitolea ufafanuzi katika mkutano uliofanyika Kijijini hapo hivi   karibuni.
Wakizungumza   na waandishi wa habari mjini Mbalizi leo, wananchi ambao waliomba   hifadhi ya majina yao walisema kuwa wanamuomba Mkuu wa mkoa wa Mbeya   kuingilia kati shida ya maji inayoukabili mji huo ili kuwanusuru na hali   mbaya ya ukosefu wa maji ambayo kwa sasa hununua lita 20 kwa Shilingi   1500 maji ambayo yanatoka Jijini Mbeya.
  Wakati   FFU wakiwa wanazunguka katika mji huo kuhakikisha hazitokei vurugu,   wananchi kadhaa walionekana wakigombania matone ya maji yaliyokuwa   yamepelekwa eneo la Tazara na Shirika la Tanzania na Zambia.
Kwa   mujibu wa baadhi ya maafisa wa Tazara ambao walihojiwa na mtandao huu   wamesema kuwa maji hayo ambayo yalikuwa ndani ya behewa moja la gari   moshi(Treni) yalikuwa maalum kwa ajili ya familia za wafanyakazi wa   Tazara wanaoishi katika Mji huo lakini wananchi baada ya kuona hivyo   wakajikusanya na kuanza kuchota maji hayo.
Hali   hiyo ilianza majira ya saa kumi jioni Novemba 13 mpaka jana majira ya   saa Nne asubuhi ambapo maji yalikuwa yamekwisha lakini imeelezwa kuwa   baada ya kuona hivyo Serikali imeamua kuwaangukia Tazara ili waendelee   kuwapelekea maji wananchi hao ili kuinusuru Serikali kuingia katika   vurugu na wananchi hao.
Novemba   9, mwaka huu wananchi hao walimtaka Rais Jakaya Kikwete kumfuta kazi   haraka ama kumwondoa wilayani humo Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Juliana   Malange kutokana na kushindwa kudhibiti genge la waporaji wa miradi ya   wananchi.
 Hayo   waliyasema katika mkutano wa hadhara uliokuwa umeitishwa na Mkuu wa   wilaya hiyo Evance Balama kwa nia ya kutatua kero ya maji ambayo   wanatozwa  kwa amri Shilingi Elfu kumi na Mamlaka ya maji iliyopelekwa   kinyemela na Serikali kijijini hapo huku kikao hicho kikishindwa kutoa   majibu kwa wananchi.
Wananchi   hao walimweleza Mkuu huyo wa wilaya kuwa tatizo hilo limesababishwa na   Mkurugenzi huyo ambaye amekiweka Kijiji hicho kama shamba la Bibi la   kuchumia fedha bila kushirikiana na wananchi huku akitumia wapambe wake   kupora miradi ya wananchi na kujimilikisha ukiwemo mradi huo.
Baadhi   ya mabango hayo yaliandikwa ‘’Tumechoka na bili hewa, ,Hivi maji ni ya   Minja na Mkurugenzi, Minja + Gadafi= na uuaji, Wazee wetu walichimba   mitaro, Minja tupe maji yetu’’
  Wananchi   hao zaidi ya Elfu ishirini waliokusanyika katika viwanja vya mahubiri   kutoa kero zao walimuuliza Mkuu huyo maswali zaidi ya ishirini ambayo   yote hayakupatiwa majibu badala yake Mkuu huyo wa wilaya aliomba radhi   kwa yale yote waliyotendewa wananchi kabla na baada ya kuhamishiwa yeye   katika wilaya hiyo.
Naye   Elia Kabholile alisema kuwa alishangaa kuona Mkurugenzi ameambatana na   Mkuu wa wilaya wakati alikuwa ameitwa na wananchi akawapuuza  kutokanana  hulka yake ya kuwa na kiburi.
Baada   ya hapo Mkuu wa wilaya alimwita Mkurugenzi wake Juliana Malange ili   ajibu yale yanayomuhusu na shutuma alizokuwa akitupiwa ana kwa ana na   wananchi hali iliyozua mtafaruku baada ya Mkurugenzi huyo kukataa kujibu   shutuma zake akiwa juu ya jukwaa la meza.
Kutokana   na hali hiyo huku wananchi wakimtaka apande katika meza iliyokuwa   ikitumiwa na viongozi wenzake kujibu hoja na kuhoji ndipo akaanza   kubembelezwa na viongozi wenzake huku akizomewa na wananchi wakisema   kuwa amekuwa shalobalo hivyo aondoke.
Hali   hiyo ilileta mzozo mkubwa, huku Mkuu wa wilaya hiyo akiamua kuchukua   makarabrasha yake na kuondoka bila mkutano kufungwa huku wananchi   wakiendelea kumzomea Mkurugenzi na kutaka kumpiga mawe Meneja wa maji   Andason Minja waliyemwita ‘’Ninja’’ aliyekuwa amefishwa katika gari STK   7534 huku msafara huo ukiokolewa na Polisi waliokuwa wakiongozwa na   Kamanda wa polisi wa wilaya hiyo Silvester Ibrahim.
Kutokana   na ubabe huo wa baadhi ya watendaji wa Serikali ya wilaya hiyo kupora   mradi wa maji, hivi karibuni wananchi wa Kijiji hicho walifunga ofisi  za  mamlaka hiyo ambayo mpaka sasa haijafunguliwa mpaka hapo mradi   utakaporejeshwa mikononi mwa Serikali ya Kijiji.
No comments:
Post a Comment