Na Esther macha, Mbeya
MWENYEKITI wa chama cha kuweka na kukopa Saccos wilaya ya mbeya vijijini Bw. Frank Phili amewataka wazazi kulipa ada za watoto wao kwa wakati badala ya kukimbilia kutoa misaada makanisani wakati watoto wao wanafukuzwa mashuleni kutokana na kukosa ada.
Akizungumza wakati wa mahafali ya pili ya shule ya sekondari ya Itebwa mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa shule hiyo na kuwashirikisha wazazi na walezi kutoka maeneo mbali mbali.
„Tunafurahi shule yetu ikiwa na mahafali mazuri kama haya kikubwa wazazi tutotoe ada kwa wakati ili ziweze kusaidia kulipa walimu lakini cha kushangaza hali hiyo imekuwa tofauti kwa wazazi kwani weamekujwa wasumbufu kulipa ada”alisema mwenyekiti huyo.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na kucheledwa ada za watoto wao kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya shule kwani walimu wanashindwa kulipa mishahara ya walimu .
Alisema kuwa ni aibu kwa wazazi au viongozi kukimbilia kutoa fedha au misaada makanisani wakati watoto wao wanafukuzwa ada mashuleni hili jambo ambalo linaumiza sana hivyo ni muhimu kwa wazazi kuzingatia hili ili kuboresha elimu kwa watoto wao.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa hata katika shule ni muhimu kuchangia ada za watoto wao ingawa hata makanisani ni muhimu kuchangia lakini elimu inatakiwa kupewa kipaumbele zaidi kwani watoto wamekuwa wakifukuzwa shule ukiuliza sababu ni ada.
„Juzi juzi tu nimeona Mbunge mmoja wa viti maalumu akitoa fedha na vifaa vya muziki kanisani lakini pia wajaribu pia kukumbuka pia hata kwenye mashirika binafsi kama haya kuchangia vifaa vya maabara”alisema. Bw. Phili.
No comments:
Post a Comment