Na Francis Godwin,Iringa CHAMA cha mpira wa miguu Manispaa ya Iringa (IMDFA) kimepata viongozi wake wakataoongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mine huku katibu msaidizi wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa (IRFA) Ramadhan Mahano akichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho. Katika uchuguzi huo uliofanyika juzi mjini Iringa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa IMDFA walimpitisha kwa kura zote za ndio Eliud Mvella ‘Wamahanji’ ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa mjini na katibu mkuu wa IRFA mkoa wa Iringa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa. Hata hivyo Mahano aliweza kuibuka na ushindi wa kishindo wa kura 31 kati ya kura 36 zilizopigwa huku mpinzani wake akiambulia kura 2 pekee na kura 3 ziliharibika. Wengine waliochaguliwa ni pamoja na Makamu mwenyekiti John Ambwene aliyepata kura za ndio 34 kati ya 36 zilizopigwa huku nafasi ya katibu ikirudi kwa mara nyingine tena kwa Bakari Kamtande aliyejizolea kura zote 36 zilizopigwa. Huku wajumbe wakimchagua mwanaharakati wa michezo katika mkoa wa Iringa Rashidi Bilo Zongo kuwa katika msaidizi wa chama hicho kwa kupata kura za ndio 34 kati ya 36 Akizungumza baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa IMDFA Mahano alisema kuwa kazi kubwa iliyopo mbele yake ni kuhakikisha soka la Manispaa ya Iringa linasonga mbele na kuwataka wadau wa soka kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wapya . Katika hatua nyingine Mahano alitaka wanamichezo ndani ya Manispaa ya Iringa kujitokeza kujaza nafasi zilizowazi hadi sasa ili kuweza kujaza safu ya uongozi katika chama hicho. Mahano alishukuru wapiga kura kwa kuonyesha kumkubali na kuahidi kuleta mabadiliko makubwa, pia alisema nafasi zilizo wazi zitajazwa mkutano mkuu ujao Alizitaja nafasi hizo kuwa Mjumbe wa kamati mtendaji 1, mwakilishi wa wanawake na mweka hazina. |
Wednesday, October 5, 2011
Chama cha Mpira Iringa chapata Viongozi wapya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment