NAIBU waziri wa Elimu na mafunzo Bw. Philipo Mulugo amewataka wananchi wa Jimbo la Songwe kupanda mazao ambayo yanavumilia ukame ili kukabiliana na baa la njaa ambalo linaweza kujitokeza kutokana na kutonyesha kwa mvua.
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mkwajuni mwishoni mwa wiki Naibu Waziri ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Songwe alisema kuwa wananchi wanatakiwa kutambua kuwa mazao ambayo yanavumilia ukame katika maeneo wanayoishi ili kusiwepo na njaa.
Alisema kuwa kila kaya inatakiwa kupanda hekali moja ya mtama au ufuta ambayo yamekuwa yakivumilia ukame tofauti na mahindi ambayo hayawezi kustahimili hali ya ukame.
Naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songwe alisema kuwa lengo la kutoa wito huo ni tahadhari kuwa huenda baadhi yakakubwa na uhaba wa mvua kulingana na hali halisi ya maeneo hayo hivyo ni lazima wananchi watambue aina ya mazao ya kulima ambayo yanastahimili ukame.
„Mnapoishi katika maeneo yenu lazima mtambue aina za mazao ya kulima ili kuweza kujiepusha na adha ya tatizo la njaa ambalo linaweza kujitokeza kwa hapo badae ni muhimu kuchukua tahadhali mapema ndugu zangu wananchi „alisema Mbunge huyo.
Akizungumzia kuhusu zao la Ufuta Bw. Mulugo alisema ni zao ambalo linakubali sana kwa jimbo la Songwe hivyo hata wananchi wakilima kwa wingi ni rahisi kuuza kwani ni zao ambalo linauzika sana hata mwananchi akilima hiloana uwezo wa kuuza na kununua mahindi kwa zile sehemu ambazo zimekubali mazao hayo.
„Niwasihi ndugu zangu watendaji wa vijiji na kata na wenyeviti wa vijiji kuhamasisha wananchi kulima mazao ambayo yanastahimili ukame n a si kupenda kulima mazao ambayo hayana uvumilivu wa ukame , hakikisheni hili linafanikiwa viongozi wenzangu hili suala la njaa ni muhimu kulifanytia kuwaelimisha watu iwapo tutafanya kazi kwa juhudi na ushirikiano toka kwa wananchi wetu”alisema.
No comments:
Post a Comment