Hivi ndivyo taka zinavyohifadhiwa pasipo kufuata utaratibu wa kuzitumbukiza ndani.
=====
Na mwandishi wetu
Wananchi wa kata ya Ilemi jijini Mbeya wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na uchache wa madampo ya kuhifadhia taka hali inayowalazimu wakazi wa eneo hilo kutupa taka ovyo.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Bi. Eva Kelioni amesema kutokana na uhaba huo wa madampo, wakazi wamekuwa wakitupa taka katika mitaro ya kupitishia maji taka na mto Magege.
Ameongeza kuwa licha ya dampo la kuhifadhia taka kuletwa bado baadhi ya wakazi wa kata hiyo wamekuwa wakitupa taka pembezoni mwa dampo hilo hali ambayo inawawia vigumu watu wa usafi kutoka halmashauri ya jiji kuondoa taka hizo kwa wakati muafaka.
Wakati huo huo amewaonya wananchi wanaoishi pembenzoni mwa mto Magege kutotupa taka kwenye mto huo ili kuondoa mazalia ya mbu ambao wanaweza kusababisha ugonjwa wa maralia.
No comments:
Post a Comment