Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, October 13, 2011

CHADEMA MBEYA WAMTAKA MEYA WA JIJI HILO ACHUNGUZWE NA KUJIUZULU

Mstaiki meya wa jiji la Mbeya Atanasi Kapunga

SAKATA la Wabunge na madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana kususia kikao cha baraza la madiwani na kuamua kutoka nje limechukua sura mpya baada ya uongozi huo kumtaka waziri wa TAMISEMI  kuingilia kati sakata la Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga kuidhinisha zaidi ya sh. Mil.4 kwa ajiri ya kulipa posho tume teule iliyoundwa  na meya ili kufanya uchunguzi wa madiwani wawili wa CHADEMA.

Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari leo katika ofisi za Chama hicho zilizopo eneo la forest,Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA ) Mbeya Mjini John Mwambigija amesema kuwa tume hiyo haikuwa na  hadidu rejea kwani iliundwa kinyume cha  kanuni za kudumu  za jiji la Mbeya .

Amesema kuwa tume hiyo haikuwa inaongoza vikao vya baraza la madiwani  na kwamba  kamati hizo zilikuwa ni za chama cha mapinduzi na zililenga kuwanufainisha kiuchumi.

Mwambigija amesema posho walizopatiwa wajumbe hao zilikuwa kwa ajiri ya kuwachunguza madiwani  wawili wa CHADEMA) ambao ni Diwani wa Mwakibete  Lukas Mwakipiki, Boidy Mwambulambo wa kata ya Forest.

Aidha amesema kitendo hicho meya wa Jiji la Mbeya kimeonyesha kumburuza Mkurugenzi wa Jiji la mbeya kwa kutumia  vibaya fedha za walipa kodi kwa kufanya mambo atakavyo ambapo alikiuka kanuni  za kidumu.

Kwa upande Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Mbeya Naomi Mwakyoma  amesema kuwa kutokana na mazingira ya uendeshaji wa vikao vya baraza la madiwani Jijini Mbeya kugubikwa na siasa za maji taka  wamesema hawana imani na utendaji  kazi meya kwa kuwa amekuwa akiendesha vikao kwa ubabe.


 Habari  na Pastor Kalulunga 

No comments: