Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, October 13, 2011

BREAKING NEWS.......WANACHUO WA TEKU MBEYA WAMEANDAMANA KUDAI MIKOPO

Wanachuo cha Teku Wakielekea ofisi za Mkuu wa mkoa jijini Mbeya
Jeshi lapolisi likiwa katika ulizi mkali wakati wanafunzi hao wakiwa ofisi za mkuu wa mkoa Mbeya

Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo kikuu cha TEKU akielezea kilicho wafanya wafike eneo hilo la kwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Wananachuo hao wakielekea ofisi ya mkuu wa mkoa Mbeya
Rais wa Teku na Waziri mkuu wake wakipigwa stop na askari wa kutuliza ghasia kuingia katika ofisi ya mkuu wa mkoa Mbeya
Wakuu hao wakiwa hawaamini kuwa wamekataliwa kuingia ofisi ya mkuu wa mkoa Mbeya
Huku wanachuo wenzao wakiwatazama kwa hasira wawakilishi wao
Mambo hayo
Haya ni Baadhi ya mabango ambayo yalikuwa yanaelezea hisia za wanavyuo hao walioandamana kutaka hatima ya mikopo yao.

Na Mwandishi wetu Joseph Mwaisango 
WANACHUO 4500 wanaosoma katika chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU) kinachomilikiwa na Kanisala la Moravian Tanzania kilichopo Jijini Mbeya wamendamana mpaka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya kueleza  yanayowapata baada ya kukosa mikopo yao.
Maandamano hayo yaliyoanzia chuoni hapo yalidumu kwa muda wa dakika 37 mpaka kufika ofisi hiyo ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya ambapo walipokaribia walizuiwa na kikosi kazi cha Jeshi la Polisi kikiwa ndani na nje ya magari PT 2079 na PT 0796.
Baada ya kuzuiwa wanachuo hao ambao walifanya maandamano ya Amani waliwaambia waandishi wa habari waliofika eneo hilo kuwa nia yao ni kumweleza Mkuu wa mkoa Abbas Kandoro ama ofisi yake juu ya kukwama kwa jitihada zao za kufuatilia mikopo hiyo.
Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Ambukege Imani alisema kuwa wanachuo hao walifanya jitihada za kupata kibali juzi kupitia jeshi la polisi ambalo lilikataa kuwapatia kibali hicho, na kwamba zaidi wanachuo hao wameshitushwa na taarifa iliyotoka bodi ya mikopo kuwa hawataweza kuwapa mikopo yao mpaka ifikapo mwezi Desemba 12 mwaka huu.

‘’Tulifanya jitihada za kuomba kibali cha maandamano lakini Polisi walikataa na viongozi wachache tulipoamua kuja kumuona Mkuu wa mkoa wenzetu wamekataa kubaki ndiyo maana wamefika hapa lakini yote ni kudai haki na tatizo ni majibu tunayoyapata kutoka bodi ya mikopo’’ alisema Rais Huyo.
Naye Waziri wa mikopo wa chuo hicho Mwilenga Lucas alisema kuwa kutokana na kucheleweshewa mikopo hiyo wanachuo wana hali mbaya ya kimaisha hivyo majibu yasiyoridhisha kutoka bodi ya mikopo ndiyo yanawalazimisha wanachuo hao kufikia hatua hiyo ya kutaka kujua ni nini kinaendelea.



No comments: