Mbunge wa jimbo la Mbarali(kushoto) Mwalimu Dickson Kilufi akisikiliza jambo kutoka kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania daima, Bwana Gordon Kalulunga mara baada ya mbunge huyo kuachiwa kwa dhamana na mahakama ya Hakimu mfawidhi wa wilaya ya Mbeya ambapo alipandishwa kizimbani mwanzoni mwa wiki hili.
Mbunge wa jimbo la Mbarali Mwalimu Kilufi(katikati), akisalimiana na baadhi ya wananchi waliofika mahakamani kusikiliza kesi ya mbunge huyo, ambaye ameachiwa kwa dhamana na mahakama ya Hakimu mfawidhi wa wilaya ya Mbeya ambapo alipandishwa kizimbani mwanzoni mwa wiki hili.
Wananchi wakiwa nje ya mahakamani baada ya kumalizika kwa kesi ya Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mwalimu Kilufi aliyeachiwa kwa dhamana na mahakama ya Hakimu mfawidhi wa wilaya ya Mbeya ambapo alipandishwa kizimbani mwanzoni mwa wiki hili.
Baadhi ya Wananchi wakitoka nje ya mahakamani baada ya kumalizika kwa kesi ya Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mwalimu Kilufi aliyeachiwa kwa dhamana na mahakama ya Hakimu mfawidhi wa wilaya ya Mbeya ambapo alipandishwa kizimbani mwanzoni mwa wiki hili.
*****
Na mwandishi wetu
Mbunge wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya Modestus Kilufi mwenye umri wa miaka 51 kupitia tiketi ya CCM aliyepandishwa kizimbani mwanzoni mwa wiki hii katika Mahakama ya Hakimu mfawidhi wa wilaya ya Mbeya na kunyimwa dhamana amechiwa huru kwa dhamana.
Kilufi aliachiwa kwa dhamana jana asubuhi na mahakama hiyo na kuamuliwa kufika Mahakamani hapo Octoba 24 mwaka huu kuendelea kusikiliza shitaka linalomkabili la kutishia kuua.
Zaidi ya wananchi 25 walijitokeza kwa ajili ya kumdhamini Mbunge huyo lakini mahakama ilihitaji wadhamini wawili tu ambapo baada ya kuachiliwa huru, nje ya mahakama kulitawala shangwe huku wakili wake Simon Mwakolo akikataa kuzungumza na waandishi wa habari na kumkataza mteja wake kuzungumza lolote.
Baada ya hapo Mbunge huyo aliwaeleza wananchi hao na familia yake kuwa alikuwa ameitwa na uongozi wa CCM kauli iliyopingwa vibaya huku baadhi wakisikika kuwa walikuwa wapi kumsaidia tangu awali na walikuwa wanamwitia nini! Hali iliyoonesha kumkatisha tamaa na baadaye alipanda gari yake na kuondoka na kwenda ofisi za chama hicho.
Awali Mbunge huyo alifikishwa mahakanani kwa kosa la kumtishia kumzuru Jordan Masweve March 16 mwaka huu wilayani Mbarali.
Kosa hilo lilielezwa kuwa ni kinyume na kifungu cha sheria 189 cha mabadiliko ya sheria ya mwaka 2002 kifungu kidogo cha 2(a) sura ya 16 ambapo mshitakiwa alikana shitaka.
Kesi hiyo yenye namba CC/158/2011 baada ya mshitakiwa kukana shitaka linalomkabili, ndipo wakili wa Mbunge huyo Simon Mwakolo aliiomba mahakama hiyo dhamana kwa mteja wake lakini Mahakama ilikataa kasha akapelekwa rumande ya gereza la Ruanda ambako amekaa mahabusu kwa muda wa siku tatu.
No comments:
Post a Comment