Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, September 21, 2011

UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA SONGWE MKOANI MBEYAWASUASUA KWA MONEKANO HUU TUTAFIKA. WAZIRI WA MIUNDO MBINU ALIPIGWA CHANGA LA MACHO.



  Baada ya ziara yake katika gereza hilo mbunge huyo alifanya ziara katika uwanja wa ndege wa  kimataifa wa Songwe na kuona maendeleo ya ya ujenzi wa uwanja huo ambao unatarajiwa kumalizika mwezi Desemba mwaka huu.
Mhandisi Amos Njoroge Kushoto akitoa taarifa kwa Mbunge viti maalum Dk Mwanjelwa katikati kuhusiana na maendeleo ya ujenzi wa ndege Songe mkoani Mbeya.
 Gari hili ndilo lililotumika wakati wa ukaguaji wa ujenzi huo.
Katika ukaguzi huo Mbunge alibaini kutoendelea kwa ujenzi wa majengo mbalimbali ya uwanja huo kama mnara wa kuongoza ndege , mapokezi, na zimamoto yakiwa kama maghofu kama alivyotembelea Desemba 16, mwaka uliopita na kumtaka mhandisi wa ujenzi wa uwanja huo Bwana Amos Njoroge na Ferdinand Chami wahatakishe kukamilisha ujenzi huo kama walivyomuahidi Waziri wa Miundombinu alivyofanya ziara yake uwanjani hapo.
 Mitambo ikiendelea kumimina lami katika barabara ya kurukia ndege
 Brabara ya lami ikiwa imependeza baada ya kutengenezwa

Masine zikishindilia barabara hiyo
 Amahakika zoezi la ushindiliaji lilikuwa likifanyika kwa nguvu moja na kwa umakini
 Mashine ya kumwaga lamu ikiendelea kumwaga lami

Mhandisi Njoroge alisema kuwa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 75, na nia yake ni kumamilika kama walivyoahidi kwa waziri wa miundombinu.

Wafanyakazi wakichimba mtaro wa maji
 Majengo ambayo toka Desema 16, Mwaka uliopita yalikuwa hivi hivi na hivyo hakuna jitihada zozote zilizofanyika kuendeleza ujenzi, Je?, ifikapo Desemba mwaka huu na Wahandisi waliahidi kukamiliza watakuwa wameshakamirisha kwa kiwango kinachotakiwa.

Aidha  Mbunge Dk Mwanjelwa aliridhishwa na ujenzi wa kiasi wa njia ya kurukia ndege ambapo sasa umeanza kuwekwa lami, ambapo alijionea wafanyakazi wakifanyakazi hiyo huku mitambo ikiendelea kufanya kazi kwa muda woteuwanjanihapo

No comments: