Na mwandishi wetu.
Wanahabari mkoani Mbeya wametakiwa kukumbuka maadili ya kazxi zao katika uandishi wa habari ili kuondoa tatizo la mwandishi kugeuka kuwa hakimu kupitia habari.
Rai hiyo imetolewa na Gadi Mkemwa ambaye ni Mkufunzi wa chuo kikuu cha Tumaini wakati wa mafunzo ya maadili Kanda ya nyanda za juu Kusini.
Amesema kumekuwa na tabia ya wanahabari kuandika habari zenye mlengo wa kumhukumu mtu fulani kutokana na kosa lake.
Kwa upande wake Mwanasheria wa kujitegemea Bwana Juma Thomasi amewataka wanahabari kutumia nafasi waliyonayo kushawishi Serikali kubadili vifungu vya katiba vinavyohusu uhuru wa habari kutokana na mwandishi wa habari kubanwa katika kazi yake.
No comments:
Post a Comment