Mbunge wa viti maalum mkoani Mbeya Dk Mary Mwanjelwa akimshangaa mtoto aliyejifungua akiwa na umri mdogo wa miaka 16 na kuachishwa shule, Hivyo ameitaka Sekta ya Elimu kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaosababisha wanafunzi wa kike kukatisha masomo baada ya kupata mimba.
Katikati ni Kaimu Mganga mkuu Hospitali ya Wilaya ya Mbozi Dk Yessayah Mwasubila ambaye pia ni Mratibu wa kitengo cha UKIMWI (CTC), akimpa maelezo ya Hospitali hiyo Dk Mwanjelwa.
Hawa ni Wauguzi wa Hospitali hiyo ya wilaya wakishuhudia kupokelewa kwa magodoro 57 kwa ajili ya wadi ya Wazazi na watoto iliyotolewa na Mbunge wa viti maalum Dk Mwanjelwa.
Wa pili kushoto mwenye suti ya kijivu ni Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Mbozi Bwa Levson Chilewa akishukuru mara baada ya kupokea shehena ya Magodoro.
Muuguzi Bi Monica Nsangu licha ya kustaafu lakini anaipenda kazi hiyo ameamua kuendelea kusaidia kutoa huduma.
Dr Mwanjelwa akimkabidhi magodoro Mkurungezi Mtendaji wa Wilaya ya Mbozi Bwana Chilewa magodoro 57.
Wajasiriamali wanawake wa Kijiji cha Isansa, wakiwa na bidhaa mbalimbali lakini Serikali, Taasisi za kifedha na wadau mbalimbali wawawezeshe akina mama hawa kupatiwa elimu ya Ujasiriamali na mikopo ili waweze kuzikomboa familia zao katika wimbi la umaskini.
Na sisi twaweza bwana kama unavyoniona, sikosi mkate wa kila siku na watoto waenda shule.
Dk Mwanjelwa akipokelewa na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Isansa, wilayani Mbozi.
Dr Mwanjelwa akizundua Bweni katika shule hiyo ya Sekondari na Bweni hilo lilipewa jina la MARY MWANJELWA ambalo ni jina lake kamili, Ambapo ameahidi kutoa vitanda 16 kwa ajili ya bweni hilo la wasichana.
Dr Mwanjelwa akifungua kitaambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua bweni hilo litakalo chukua wanafunzi 64 wa kike.
Bweni likiwa limeshazinduliwa na kuwataka wanafunzi hao kulitunza bweni hilo ili liweze kutumiwa na vizazi vinazyokuja.
Taswira ya mbele ya Bweni hilo lililopewa jian la Mary Mwanjelwa.
Dr Mwanjelwa akikabidhi veti katika mahafali ya 11 ya shule ya Sekondari Isansa, wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Kwa ushirikiano wa Kamanga na Matukio, Mbeya Yetu na Chimbuko Letu.
No comments:
Post a Comment