Edwin Sambala mgombea udiwani wa kata ya Gangilonga (Chadema) akiwa ameduwaa ndani ya ofisi ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata hiyo ambaye alitelekeza ofisi yake na kwenda kata ya Kitanzini
Viongozi wa Chadema mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wa kwanza kulia,mbunge wa viti malum mkoa wa Iringa Chiku Abwao mgombea udiwani kata ya Kitanzini Gervas Kalolo na katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonokulima wakimtazama msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kitanzini wakati akikagua fomu ya Kalolo
Viongozi wa Chadema mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wa kwanza kulia,mbunge wa viti malum mkoa wa Iringa Chiku Abwao mgombea udiwani kata ya Kitanzini Gervas Kalolo na katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonokulima wakimtazama msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kitanzini wakati akikagua fomu ya Kalolo
VITUKO vyaibuka zoezi la urejeshaji fomu za udiwani kata ya Gangilonga katika jimbo la Iringa mjini linaloongozwa na mbunge wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) mchungaji Peter Msigwa baada ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Gangilonga Lucas Wikes kuitelekeza ofisi yake kwa mgombea udiwani wa Chadema Edwin Sambala aliyekuwa diwani wa CCM kata hiyo mwaka 2005 hadi 2010 kabla ya kujiengua CCM na kujiunga na Chadema.
Msafara huo wa wafuasi wa Chadema na viongozi wake wakiongozwa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Msigwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwalo (chadema ) pamoja na viongozi wa wilaya na mkoa walikutana na kituo hicho majira ya saa 8 .15 hivi mchana baada ya kufika katika ofisi ya afisa mtendaji kata ya Gangilonga na kukutana na kitabu cha wageni mezani huku mhusika ambaye ni msimamizi wa uchaguzi msaidizi akiwa ameikimbia ofisi hiyo.
Kituo hicho ambacho kilionyesha kuwatibua nyongo wafuasi wa Chadema na kutaka kuifunga ofisi hiyo kimekuja huku kata hiyo ikionekana kuwa ni tete kwa ushindi wa CCM baada ya mshindi wa kura za maoni ndani ya CCM Michael Mlowe kukiumbua chama chake kwa kujitoa dakika za mwisho kugombea kabla ya CCM haijafanya uteuzi wa majina ya wagombea na nafasi yake kumpa mshindi wa pili Nicolina Lulandala ambaye alikataliwa na wana CCM katika kura za maoni.
Mmoja kati ya watumkishi wa ofisi hiyo ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Gangilonga ambaye hakupenda kutaja jina lake aliwaeleza viongozi hao wa Chadema kuwa mtendaji huyo alikuwepo ofisini kwake dakika 10 zilizopita na baada ya kusikia shamla shamla za Chadema zikikaribia ofisi hiyo alilazimika kutoweka ofisini kwake na kuacha kitabu cha wageni na kusahau koti lake katika kiti na kutoweka kusiko julikana.
Wakizungumzia tukio hilo wabunge wa Chadema Mchungaji Msigwa na Abwao walisema kuwa tukio hilo linafanana kabisa la lile la mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ambao ulipelekea CCM kushindwa vibaya katika uchaguzi huo.
Abwao alisema kuwa CCM imekuwa na kawaida ya kuandaa mazingira ya uchakachuaji wa matokeo toka mwanzo na kuwa hata kutokuwepo kwa msimamizi huyo ofisini na njama za CCM kutaka kuvuruga zoezi hilo kama ilivyotaka kufanya mwaka jana kwa kumzuia aliyekuwa mgombea urais wa Chadema Dkr Slaa kuhutubia katika viwanja wa Mwembetogwa kwa kuwatoa wanafunzi wa sekondari ya wazazi wa CCM Mwembetogwa kuigiza kufanya bonanza la kusaka vipaji katika uwanja huo hali iliyoamusha jazba kwa wananchi na kutoa hukumu dhidi ya CCM.
Hata hivyo alisema kuwa Chadema imejipanga kukabiliana na vituko vyote vya CCM katika uchaguzi huo ambao ushindi kwa Chadema upo wazi kwa kata zote.
Huku Mbunge Msigwa akidai kuwa tayari amewasiliana na msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini kumjulisha juu ya tukio hilo na kuwataka wana Chadema na wananchi kukumbuka kutoka hukumu kwa CCM siku ya uchaguzi.
Hata hivyo katika hali ya kujiami na njama hizo za kuachiwa ofisi viongozi hao wa Chadema walilazimkika kumwacha mgombea udiwani wa kata ya Gangilonga Samba na wafuasi wawili pekee ndani ya ofisi hiyo na msafara mkubwa uliokuwa umewasindikiza wagombea hao wa udiwani kata ya Gangilonga na Kitanzini Miyombini kuondoka eneo hilo na kwenda kata ya Kitanzini kwa ajili ya kumsindikiza mgombea wao Gervas Kalolo kurudisha fomu ambako nje ya ofisi ya msimamizi msaidizi wa kata ya Kitanzini Miyomboni walishangazwa kumkutana Lucas Wikes ambaye ni msimamizi msaidizi wa kata ya Gangilonga aliyetelekeza afisi yake kitendo kilichowatibua zaidi wafuasi wa Chadema na kutaka kumpa kichapo kiongozi huyo.
Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonokulima alieleza kusikitishwa kwake na hatua ya kukosekana kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika kata ya Gangilonga na kuwa chama chake kinajipanga kufikisha malalamiko kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi.
Huku Wikes akijitetea juu ya kutokuwepo ofisini kuwa alilazimika kuondoka ofisini baada ya yeye kuwekewa pingamizi la kuwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika kata hiyo na hivyo kuondoka kwake ni sahihi kwani hata angekuwepo asingeweza kupokea fomu hiyo.
Kwa upande wake msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini Teresia Mahongo alisema kuwa kukosekana kwa msimamizi huyo msaidizi kwa leo si kosa kwani siku ya mwisho kurejesha fomu ni kesho ambapo wasimamizi wasaidizi wa vkituo vyote viwili hawatatakiwa kuondoka hata sekunde moja katika vituo hadi muda wa mwisho wa kurejesha fomu uliopangwa na tume ya uchaguzi ya Taifa.BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment