Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, September 9, 2011

WAKAZI WA MWAKIBETE JIJINI MBEYA WALIA NA WANAOTUPA TAKA ENEO LISILO RASMI.

Na mwandishi wetu.
Wakazi wa mtaa wa Nyibuko kata ya Mwakibete wamewalalamikia baadhi ya wakazi wa maeneo ya jirani kwa kitendo cha kutupa taka eneo lisilo rasmi.

Wakiongea na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti bwana Abasi Kalinga na Bi Albina Masheta wamesema kuwa licha ya kukatazwa kutupa taka eneo hilo watu hao wanaendelea kutupa taka hizo hasa nyakati za usiku .

Kwa upande wake afisa mtendaji wa mtaa huo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu maalum amesema kuwa huwa wanafanya mikutano kila wakati kuzungumzia mazingira yao na kwamba waliweka vibao vya matangazo kuwataka watu kuacha kutupa taka katika eneo hilo.

Pia ameongeza kuwa wanampango wa kumtafuta mgabo wa kulinda eneo hilo ili waweze kuwakamata watu hao na kuwafikisha mbele ya sheria.

No comments: