Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, August 10, 2011

Tamasha La Tigo Jijini Mbeya Funika Bovu Nature,Roma na wasanii kubao wakonga nyoyo za wanambeya

 
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature akitoa burudani katika viwanja vya Nane Nane mjini Mbeya hivi karibuni katika tamasha maalum lililoandaliwa na kampuni y simu za mkononi ya Tigo.

Umati wa watu kibao wakishuhudia Tamasha hilo
Roma akipagawisha jukwaani wakati wa Tamasha hilo la Tigo Jijini Mbeya

 Kiduku nao walisimama vilivyo katika tamasha hilo la tigo
Meneja wa mauzo mikoa ya Mbeya na Rukwa Kevin Mibazi (kulia) akimkabidhi zawadi ya simu ya mkononi mmoja wa washindi wa kusakata kiduku Monica Jonas.

Nature afunika Tamasha la Tigo Mbeya

Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi kipya kutoka jijini Dar es Salaam, Juma Nature juzi alikonga nyoyo za washabiki wa  muziki huo vilivyo katika tamasha maalum lililoandakiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Nane Nane mjini Mbeya.

Katika tamasha hilo ambalo lilifanyika katika viwanja vya Nane Nane mjini humo, Nature alipanda jukwaani akiwa na baadhi ya wanamuziki wengine wanaounda kundi la TMK Wanaume Family kwa kuanza kuimba nyimbo mbalimbali ambazo aliwahi kutamba nazo miaka ya nyuma kama vile Zali la Mentali, Mtoto Idi na nyinginezo.

Kadri alivyokuwa akizidi kutoa burudani ndivyo washabiki walivyokuwa wakipandwa na mzuka hadi kufikia hatua ya kukata uzio uliokuwa mbele ya jukwaa huku kila mtu akitaka kumshika mkono. Hali hiyo ilisababisha Nature kusimamisha burudani kwa dakika kadhaa ili kurudisha hali ya utulivu na hatimaye burudani ilirejea katika hali yake ya kawaida.

Mbali na Nature na kundi lake la TMK Wanaume family, mwanamuziki mwingine aliyeonyesha uwezo mkubwa jukwaani katika stahili ya muziki wa kizazi kipya kutokana na kushangiliwa na umati kila mara ni Roma Mkatoliki kutoka Tanga ambaye alipanda jukwaani baada ya Nature na kundi la TMK Wanaume family kumaliza kutoa burudani.

Akiongea baada ya Tamasha hilo Meneja wa Mauzo wa Tigo wa mikoa wa Mbeya na Rukwa Kevin Mibazi alisema kuwa mbali na kuadhimisha sikukuu za Nane Nane, tamasha hilo pia lilikuwa la kuwashukuru  wateja wa Tigo kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani.

”Ndiyo maana katika tamasha ili tumeamua kutoa huduma zetu kwa bei ya chini ili kila mtu apate huduma zetu kwa bei inayo kubalika, kwahiyo tunatumia fursa hii kuleta burudani ya wasanii wakubwa, na kama ulivyoona wanapendwa sana kama kuwashukuru wateja wetu,” alisema Mibazi

Katika tamasha hilo wateja wa Tigo walipata hudum mbalimbali kama vile hudfuma ya Tigo pesa, Tigo intaneti, kusajili laini mpya za simu ,Tigo rusha. Halikadhalika kulikuwa na simu ambazo ziluzwa kwa bei ya punguzo.

Kwa mujibu wa Mibazi matamasha kama hayo yameishafanyika katika baadhi ya mikoa na yanatarajiwa kuendelea  katika mikoa mingine hapa nchini kama sehemu ya kuhamasisha huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni ya Tigo.

No comments: