Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, August 10, 2011

MALALAMIKO YA WANANCHI WA MIVUMONI KUHUSU UHARIBIFU WA MAZINGIRA YA MAKAZI YA WATU



Asalaam Aleykum,
Ni matumaini yetu kuwa unaendelea vema na shughuli zako za kila siku pamoja na kuliendeleza libeneke. Hongera tena kwa kazi nzuri ya kuihabarisha jamii kupitia Blog yako ya jamii.

Tunaomba utusaidie kuwahabarisha WAHUSIKA na wenye MAMLAKA juu ya KERO yetu kubwa ya wachimba mchanga katika maeneo yetu. Tulikwishatoa taarifa juu ya jambo hili miezi miwili iliyopita lakini bado inashangaza kuona jambo hili lauharibifu likiendelea.

Hivi ni kwa nini katika nchi hii baadhi ya WATENDAJI huwa wanapopewa taarifa ya swala linalogusa maisha ya wengi huwa hawalifanyii kazi haraka? Ni mpaka madhara yanayotokana na wananchi wenyewe kuchukua hatua mikononi ndipo hatua zitakapochukuliwa? Au Je wanasubiri RAIS wetu ndio aje mwenyewe kutatua na kutafuta suluhisho la jambo ambalo halihitaji mkuu wa Nchi kulifanyia kazi? Inashangaza sana.

KWELI Inashangaza sana kuona sehemu iliyopimwa Viwanja na ni makazi ya watu na kuna barabara za mitaa ZILIZOGHARIMU FEDHA NYINGI za umma halafu wanajitokeza watu wachache wasiopenda MAENDELEO wanakuja KUCHIMBA mchanga na wanapoambiwa na wakazi wa eneo hili husika kwamba ondokeni watu hawa bado wanaendelea kuchimba mchanga na wala hawaogopi.

Iko hatari kubwa sana ya kuharibiwa eneo la MIVUMONI block 5 lililoko wilaya ya KINONDONI, kuna vijana wameanza kuchimba eneo lililo karibu kabisa na Transforma ya Block 5 barabara ya LAGOS ambayo ilitugharimu sana kuipata . Na zaidi sana eneo wanalochimba mchanga ni for PUBLIC use na ambalo WANANCHI wa eneo hili tunapaswa kulilinda.

Wananchi wa eneo hili tumeshafanya juhudi nyingi sana kuwafukuza lakini bado wanaendelea kuchimba. Tulipowauliza kwa nini wanachimba mchanga kwenye eneo hili ambalo ni Residential area, Wanasema na kutuuliza bila aibu kwa nini tunawazuia kufanya kazi yao?

Wananchi wa eneo hili tuliweza kuwasilisha taarifa hizi kwa ofisi ya serikali ya Mtaa wa Mivumoni , kwa DC wa Kinondoni pamoja na Municipal Director wa Kinondoni lakini bado jamaa hawa wanaochimba mchanga wanakuja usiku na malori na wanachimba na wanaendelea kuharibu mazingira. Mpaka Sasa inaonyesha hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa maana watu hawa wanaochimba mchanga bado wanaendelea licjha ya sisi wananchi wa eneo hili kutoa namba za magari yanayohusika kuchimba na kubeba mchanga katika eneo hili.

Kinachoumiza zaidi ya kuwa na HANDAKI ambalo halita weza kuzibwa leo wala kesho kutwa litakuwa ni gharama sana kwa sisi wakaazi wa eneo hili kulifukia na ni hatari zaidi pale mvua kubwa zitakapoendelea kunyesha maana inaweza kusababisha mmomonyoko mkubwa sana wa ardhi katika eneo hili.

Sio handaki tu cha kushangaza zaidi ni kwamba wanaikaribia TRANSFORMA iliyoigharimu TANESCO fedha/gharama kubwa sana kuipata na kuja kuiweka katika eneo letu la Mivumoni.

Eneo hili limeshaharibiwa sana na TAARIFA ZILITUMWA KWA VYOMBO HUSIKA TANGU MWEZI JUNE 2011 HADI HIVI LEO TAREHE 10 AUGUST,2011 HAKUNA HATUA YOYOTE ILIYOCHUKULIWA NAWATU HAWA WENYE MALORI WANAENDELEA KUCHIMBA TU NA KUHARIBU MAZINGIRA YA ENEO HILI. Ni wakati muafaka sasa kwa vyombo husika kuchuka hatua kali za kuzuia uharibifu huu mkubwa wa mazingira na kutoa ADHABU kali ikiwa mojawapo ni wale wote waliochimba mchanga eneo hili kulirudisha kama lilivyo kuwa awali.

Inashangaza kuona watu hawa wanaochimba mchanga wanaendelea KUCHIMBA MCHANGA na kuzidi kuharibu MAZINGIRA ya eneo hili. Sisi WANANCHI wa Mivumoni tunatoa tena TAARIFA hii kwa wote wanaohusika KUCHUKUA HATUA KALI kuzuia uharibifu huu kwani hivi hawa ni nani wanaendelea kuchimba mchanga eneo la makazi halali ya watu?

Na je kwa nini watu wanajifanyia mambo hovyo hovyo namna hii? Je vyombo husika vinasubiri wananchi wa eneo hili tuanze kupambana na hawa wanaochimba mchanga? Sio siku za mbali sana wananchi wa eneo la jirani ya Mivumoni walijichukulia hatua mikononi sasa tunadhani ni wakati muafaka kwa wananchi wa eneo hili pia kufanya hivyo kwa hawa wachimba mchanga.

Maana sasa hapa ndipo mahali ambapo huwa inakuwa vigumu kuwaambia watu wasichukue HATUA MIKONONI. Taarifa za jambo hili tulishazitoa na sasa sisi wananchi wa Mivumoni Block 5 & 6 tunatoa WITO kwa vyombo husika kuchukua hatua haraka kwani kinachofuata sasa ni sisi kuchukua hatua mikononi wenyewe.

Asante

Sisi Wananchi wa Mivumoni na wapenda MAZINGIRA
Habari kwa hisani ya Michuzi blog

No comments: