Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, August 16, 2011

Mkuu wa zamani Jeshi la Zimbabwe afariki dunia




Mkuu wa zamani Jeshi
la Zimbabwe Solomon Mujuru



Mkuu wa zamani wa Jeshi la
Zimbabwe Solomon Mujuru amefariki dunia kwa moto katika shamba lake,
taarifa rasmi zimeifikia BBC.


Bw Mujuru mwenye umri wa miaka 62, alikuwa
mwanasiasa mwandamizi na mume wa Makamu wa Rais wa Zimbabwe Joice
Mujuru.



Wachambuzi wanasema kifo chake huenda
kitazidisha mkanganyiko kwenye chama cha Rais Mugabe kuhusu nani
atakayemrithi kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 87.



Akijulikana kama Rex Nhongo wakati wa vita vya
msituni, alikuwa mkurugenzi wa vikosi vya Muganbe wakati wa vita vya
uhuru miaka ya 1970s’.



Afisa mmoja ameiambia BBC kuwa Jenerali Mujuru
alikufa kwa moto uliotokea katika nyumba yake ya shambani katika eneo la
Beatrice, kilometa 80 (maili 50) kusini mwa mji mkuu Harare asubuhi ya
Jumanne.



Haijulikani iwapo alikuwa peke yake wakati huo
au kama alipewa ulinzi wa jeshi.



Rais Mugabe anatarajiwa kutoa tamko rasmi
kuthibitisha kifo cha Jenerali Mujuru baadaye leo kwa mujibu wa itifaki
za chama cha Zanu-PF.



Mwandishi wa BBC Brian Hungwe mjini Harare
anasema Jenerali Mujuru alikuwa mwanachama mwandamizi wa chama cha
Zanu-PF na anaelezwa kuwa alikuwa mwenye msimamo wa kadri.



Alikuwa mpanga mikakati na kusemekana akiwa na
ushawishi mkubwa wa kuweka viongozi wenye nguvu katika siasa za Zanu-PF
, anasema.



Kifo chake kimeacha pengo na kumuuacha mkewe
bila nguzo ambaye ni mmoja kati ya makamu wawili wa Rais, wachambuzi
wanasema.



Wakati wa vita dhidi ya utawala wa Rhodesia
katika miaka ya 1970s, Jenerali Mujuru aliongoza mapambano ya silaha
pamoja na marehemu Josiah Tongogora.



Mwandishi wa BBC anasema alikuwa Jenerali Mujuru
aliyewahamasha wapigania uhuru wa Msumbiji wakati wa mgogoro kumkubali
Bw Mugabe kama kiongozi wa vikosi vya vuguvugu la waasi wa Zanla baada
ya kuachiliwa kutoka kizuizini mwaka 1974.



Wakati wa uhuru mwaka 1980 aliongoza kikosi cha
jeshi kabla ya kustaafu na kuingia katika biashara miaka 10 baadaye.



Mwandishi wetu anasema akiwa kiongozi wa
wapigania ukombozi dhidi ya utawala wa kikoloni, Jenerali Mujuru
anatarajiwa kuzikwa kwa heshma ya kitaifa, katika makaburi ya mashujaa
baadaye wiki hii.



Source: BBC SWAHILI







No comments: