Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, August 16, 2011

Vodacom Miss Tanzania wapokelewa kwa heshima Monduli


 Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Regina Lowasa pamoja na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha Namelok Sokoine wakicheza mziki wa Kwaito na Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakati wa tafrija maalum ya kuwakaribisha warembo hao katika mji wa Monduli juzi mkoani Arusha. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo. 
 Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Regina Lowasa akicheza mziki wa Kwaito na Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakati wa tafrijka maalum ya kuwakaribisha warembo hao katika mji wa Monduli juzi mkoani Arusha. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo. 
 Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa wamevalia vazi maalum livaliwalo na wanawake wa jamii ya Kimasaai wakati warembo hao na wenzao walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo. 
 Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakipakua chakula wakati wa tafrija maalum ya kuwakaribisha katika mji wa Monduli jana. Tafrija hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine na dada wa Mbunge wa Monduli Kalaine Lowasa. 
 Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao baada ya kukaribishwa katika mji wa Monduli jana katika tafrija iliyoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine na dada wa Mbunge wa Monduli Kalaine Lowasa
 Dada wa Mbunge wa jimbo la Monduli na Waziri Mkuu mstaafu Kalaine Lowasa akiwavisha warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, mgolole wa kimasai wakati warembo hao walipoandaliwa tafrija maalum ya kuwakaribisha katika mji wa Monduli.Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Arusha, Namelok Sokoine. Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine akimshika mkono mmoja wa washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania baada ya kuvishwa mgolole wa kimasai na dada wa Mbunge wa Monduli, Kalaine Lowasa (wapili kushoto) jana baada ya kuwasili Monduli. Kushoto ni Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa shindano hilo, Hashim Lundenga
 Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiangalia nyoka aina ya chatu wakati warembo hao na wenzao walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
 Mshiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, Glori Lori akiwa amejivisha nyoka shingoni huku wenzake wakimwangalia wakati warembo hao na wenzao walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
Blessing Ngowi, Mshiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, akiwa amejivisha nyoka shingoni huku wenzake wakimwangalia wakati warembo hao na wenzao walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.

===============================

 Vodacom Miss Tanzania watembelea kaburi la Hayati Sokoine
Na Mwandishi Wetu
Ziara ya mafunzo ya washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 imeendelea Mikoa ya kanda ya Kaskazini na warembo hao wamepata fursa ya kutembelea kaburi la aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine.
Wakiwa eneo la Monduli warembo hao walipokelewa na Mtoto wa Sokoine Namelok Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Arusha.
Mbunge huyo alipata fursa ya kuwapa historia fupi ya maisha ya baba yake hasa alipokuwa Waziri Mkuu,mapema walipowasili wilaya ya monduli walipokelewa na mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mama Regina Lowasa na viongozi wengine wa wilaya hiyo,Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Viti Maalum wa mkoa wa Arusha Namelok Sokoine na alipata fursa ya  kuwaasa warembo hao pamoja na ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii na maeneo ya kihistoria watumie fursa hiyo kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa elimu kwa watoto wa kike hasa jamii ya kimasai,alisema jamii ya kimasai ambayo inajishughulisha na ufugaji haijatoa kipaumbele katika kumsomesha motto wa kike hivyo ziara ya warembo hao inaweza kutumika kubadilisha mtizamo huo.
 Akizungumzia ziara hiyo Meneja Uhusiano na Habari kwa Njia ya Mtandao wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu alisema washiriki hao walijifunza vitu mbalimbali alivyovifanya Hayati Sokoine enzi za uhai wake.
Mara baada ya kutoka katika eneo hilo warembo hao 30  pia walitembelea shule ya Maasai Girls iliyopo Monduli kabla ya kupata chakula cha jioni.
“Ziara yetu bado inaendelea na warembo wanaendelea kujifunza kupitia elimu inayotolewa na wataalam mbalimbali wanaopata fursa ya kukutana na warembo wetu. Ni matumaini yetu wataitumia elimu hii kulitangaza taifa katika medani za kimataifa,” alisema Nkurlu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Lino  Agency ambao ndio waandaaji wa Vodacom Miss Tanzania Hashim Lundenga alisema warembo hao pia watatembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorogoro NCAA, ili kujionea moja ya maajabu saba ya dunia.
Akifafanua Lundenga amesema mwaka huu wanataka warembo wenye sifa ikiwemo elimu, muonekanao na tabia nzuri ili mshindi atakayepatikana aweze kutuwakilisha vema katika medani za kimataifa hususani kujua vivutio vya kitalii vilivyopo nchini.
“Baada ya kutoka Mikumi ziara hii ya mafunzo sasa imeingia kanda ya kaskazini, tukiwa safarini kutokea Morogoro warembo walipata fursa ya kupiga picha katika maeneo mbalimbali ikiwemo daraja la mto wami na mji maarufu wa Moshi mkoani Kilimanjaro,” alisema Lundenga.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wengine mrembo Jennifer Kakolaki alisema kuwa wanaifurahia ziara hiyo kwani mbali ya kujionea rasirimali tofauti zilizopo nchini wanajifunza mengi kuhusiana na utalii wa ndani.
“Kiujumla Watanzania hawana budi kutenga siku maalum katika mwaka ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini. Binafsi nimepanua kiwango changu cha ufahamu kuhusiana na utajiri wa rasilimali za taifa zilizopo nchini,” alisema Jennifer.
Mwaka huu warembo hao wameingia kambini kwa mfumo  tofauti na uliozoeleka kwani wamewekwa kwenye jumba maalum la ‘Vodacom House’ ambapo matukio yao yatakuwa yakioneshwa kupitia Startv na Clouds TV na watazamaji watapata fursa ya kupiga kura kuchagua mrembo watakayemuona anafaa.

No comments: