Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakitembelea kukagua makaburi 101 kati ya 108, ya askari ‘Mashujaa’ walifariki wakati wakipigana vita Msumbiji na kuzikwa katika Makaburi ya Naliendele mkoani Mtwara, wakati wa sherehe za kumbukumbu za Mashujaa zilizofanyika leo Julai 25, 2011 mkoani Mtwara. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
(Picha na Freddy Maro wa Ikulu)
Rais Jakaya Kikwete, akiwahutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Makaburi ya naliendele mkoani Mtwara. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakitembelea na kukagua makaburi ya Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Mashujaa iliyoadhimishwa katika viwanja vya makaburi ya Mashujaa Naliendele, mkoani Mtwara leo Julai 25, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimia wananchi katika sherehe hizo.


No comments:
Post a Comment