Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, July 25, 2011

DAWA ZA KUULIA KUPE ZATUMIKA KUHIFADHIA SAMAKI MBEYA

Mvuvi wa akiwa kazini

BIASHARA ya Samaki ni bidhaa ambayo imekuwa ikifanywa na watu wengi
hususani wanawake na ni kitoweo ambacho kimekuwa kikipendwa na watanzania
walio wengi hususani wale wanaoishi maeneo ya Ziwani kutokana na urahisi
wake wa kupata na hata unafuu wake wa upatikanaji.

Lakini hali imeanza kuzua hofu kwa walaji wa kitoweo hicho hasa
wanawake ambao asilimia kubwa ndio wamekuwa wakitegemea kuishi maisha
yao kwa kutegemea biashara hiyo kutokana na dawa inayotumika kuulia
wadudu aina ya KUPE( Accaricide) kutumika kuhifadhia samaki wabichi.

Hali hiyo imeanza kujitokeza baada ya wafanyabiashara wa Samaki katika ziwa
Rukwa kuanza kutumia dawa za Accaricide zinazotumika katika kuulia wadudu
aina ya Kupe kuhifadhia samaki ili wasiharibike.

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu kwa msaada wa Mtandao wa Kijinsia
Tanzania(TGNP)lilifanya utafiti katika maeneo ya Mwambani Wilayani
Chunya ,Kijiji cha Ihovi, na kubaini kuwa dawa hiyo imekuwa ikitumika
katika kuhifadhia Samaki wabichi
ili wasiharibike pindi wanapowasafirisha tayari kwa ajiri ya kuwauza katika
maeneo mengine nchini.

Hata hivyo mmoja wa watumiaji wa dawa hizo Bw.Levocatus Nzowa anasema
kuwa kuwa dawa hizo zimekuwa zikiwasaidia sana kuhifadhia samaki hao
licha ya kuchukua sikuchache kuishiwa makali.

“Licha ya kuishiwa makali kwa muda mrefu lakini sisi tumebaini kuwa dawa hii
inatusaidia sana sisi wafanyabiashara kutokana na hali halisi ya uchumi wetu
wa kimaisha”anasema

Aidha Bw. Nzowa anasema kuwa wanachokifanya katika matumizi ya dawa hizo ni
kwamba wanachukuwa dawa hiyo na kuweka kwenye maji ambayo yanaendana na
uwingi wa samaki na kasha kuloweka samaki kwa zaidi ya masaa mawili au
matatu .

Anafafanua kuwa dawa hiyo baada ya kuwaweka samaki hao kwa hayo masaa
inakuwa msaada mkubwa sana kuzuia ili wasiharibike mapema kutokana na wao
wafanyabishara kusafirisha mbali .

Hata hivyo mmoja wa Daktari anayeuza dawa za mifugo Jijini
Mbeya Bw.
Aidan Said anasema kuwa zimekuwa zikinunuliwa sana na wavuvi na
wafanyabiashara mikoa ya Rukwa na Mbeya.

Anasema kuwa ni miaka ya hivi karibuni wafanyabiashara wa dawa hizo waanze
kuzitumia na kudai kuwa licha ya wao kama madaktari kujaribu kuwaeleza
madhara ya dawa hizo lakini bado inashindikana kutokana na wafanyabiashara
hao kutumia kauli ya kwamba wanakwenda kuzitumia katika mifugo yao.

Aidha Dkt. Said anasema kuwa suala la kudhibiti matumizi ya dawa hizo
inatakiwa ifanywe na serikali kwa kuanzisha operesheni ya kupima samaki
wabichi kabla hawajaanza kuuzwa kwenye masoko yote nchini ili kubaini
wanaotumia dawa hizo.

Hata hivyo anasema kuwa kimsingi dawa hizo ni sumu kwa walaji wa samaki
lakini itakuwa vigumu sana kwa wao kuwazuia wasinunuwe dawa kwao kwa kuwa
matumizi ya dawa hizo yanaeleweka lakini kutokana na kuwepo kufoji kwa dawa
sio jambo lahisi kuwakataza.

Akizungumzia matumizi mabaya ya dawa hiyo Ofisa kilimo na mifugo wa Mkoa wa
Mbeya Bw.Wilfred Kayombo anasema kuwa matumizi mabaya ya dawa ni
kutokana na kukosekana kwa elimu kwa watu waishio vijijini na kudai
kuwa wengine
wamekuwa wakichukulia kama ni jambo la kawaida hata wakiwa kwenye familia
zao.

Aidha Kayombo anasema kuwa yote hayo yanatokana na ugumu wa maisha
ambapo anasema jamii inajaribu kutumia njia za mkato kurahisisha mambo
ndiyo maana hata wengine wamekuwa wakitumia hata vidonge vya panado
badala ya viwili
wanatumia vinne.

Naye Ofisa Afya wa Mkoa wa Mbeya Bw.Peter Mereki anasema kuwa dawa za
Accaricides ni sumu ambayo inaingia kwenye ngozi ya mifugo pindi inapotumika
hivyo kinachofanyika ni pale wadudu au Kupe wanapojaribu kunyonya damu
wanakunywa hiyo dawa na
kufa.

Anasema kuwa kwa upande wa samaki kinachofanyika ni ile sumu kuingia kwenye
minofu ya samaki nakubainisha kuwa iwapo mtu ataweza kula samaki aliyewekwa
kwenye hiyo dawa lazima atakuwa amekula sumu.

Anabainisha kuwa dawa licha ya kuingia kidogo kwenye mwili wa binadamu lakini
anasema madhara yake ni makubwa ambayo ni pamoja na magonjwa mbali mbali
ikiwemo saratani au vifo vya ghafla.

Bw.Mereki anasema watu wanaofanya vitendo hivyo ni sawa na majambazi ambao
wanakusudia kuuwa jamii isiyo kuwa na hatia nakuongeza kuwa lazima serikali
ifanye jitihada za ziada kwa kuwa samaki ni chakura kinachotumika na watu
wengi nchini.

Anasema sumu itokanayo na dawa za kupe inaweza ikatambulika baada ya miaka
mtano hadi ishilini ambapo anasema kwa mtumiaji hawezi kutambua ugonjwa huo
aliupata katika mazingira gani, nakuongeza kuwa hata vifaa vya kuweza
kutumika kubaini magonjwa hayo huwenda vikashindwa kubaini ndipo mtu anaweza
kufa kifo cha ghafla.

Hata hivyo kwa upande wao wavuvi wa Samaki katika Ziwa Rukwa katika Kijiji
cha Ihovi Wilayani Chunya wanasema kuwa walikuwa hawafahamu kama
dawa hiyo ina madhara kwa afya ya binadamu lakini kwao ndio n njia
rahisi kwao ili
samaki wasiweze kuharibika tofauti na matumizi hayo hupata hasara kubwa ya
samaki wao kuoza.

Mama Mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mama John Mkazi wa Kijiji cha
Miembeni kata ya Saza anasema kuwa wao kama wafanyabiashara wa samaki
dawa hiyo imekuwa ikiwasaidia kwa kiasi kikubwa licha ya kuwa
inahifadhi kwa muda
mchache lakini imekuwa mkombozi kwao.

“Ugumu wa maisha ndio unatufanya tutumie dawa hizi mimi hapa nilipo sina
mume na nina watoto wane wote wananitegemea mimi kwanza sijui hata
kama
kuna madhara katika dawa hizi tunatumia tu labda kama
tungepatiwa elimu huku
vijijini tungeweza kufahamu madhara yake lakini bila ya hiyo sisi
tutaendelea kutumia tu”anasema Mama John.

Kwa kawaida mimi hawa samaki wangu nawachukua sasa Ziwani na kusafirisha
mpaka wafike huko wanakokwenda inanilazimu nitumie dawa hii vinginevyo
nitapata hasara kwani wataoza wote njiani njia rahisi ni hii tu”anasema.

Kwa upande wake Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mwambani
Dkt.Kusenge Benangodi anasema kuwa matumizi ya dawa hiyo kuhifadhia
samaki ni hatari kwa binadamu kwani inaweza kusababisha kupata
Kansa,, Kuvimba ini, na kuwa hata kwa wanawake inaleta madhara
makubwa sana kwa upande wa uzazi kwani kwa hapo baadaye mwanamke
anaweza kupata ugonjwa wa kifafa cha mimba na magonjwa mengine ya
wanawake.

“Ni jukumu la serika pamoja na mamlaka ya chakula na dawa kutoa elimu kwa
wafanyabishara kujua madhara ya matumizi ya dawa hiyo na Mamlaka ya chakula
na dawa inatakiwa kuingilia kati matumizi ya ya dawa hiyo kwani ina madhara
ambayo si mazuri sana”anasema

Dkt.Benangodi anasema kuwa baada ya miaka 10 kunaweza kukatokea madhara
makubwa na serikali inatakiwa kufanya jitihada kufanya uchunguzi wa dawa
hii kwa matumizi ya samaki .

“Utoaji wa elimu hiyo uanzie maeneo ya vijijini kwani wanawake wengi waliopo
vijijini hawafahamu matumizi mabaya ya daa hiyo na hata madhara yake hivyo
kuna uwezekano mkubwa kwa wanawake wea vijijini wakapata madhara hayo kwani
wao wanatumia tu lakini athari zake hawahafamu “anasema.

Kwa Upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dkt. Wedson Sichalwe
anasema kuwa suala
hilo la matumizi ya dawa hiyo katika kuhifadhia
samaki hana taarifa isipokuwa atafanya mawasiliano na kikosi kazi
cha cha mabwana afya
wa Wilaya ili waweze kujua undani wa matumizi ya dawa hiyo na kulitolea
taarifa mapema.

Hata hivyo Mganga Mkuu huyo anabainisha kuwa matumizi ya dawa hiyo ni
mageni
kwake lakini atafanya jitihada za haraka ili kutuma kikosi kazi chake
cha wataalamu wa afya

Imeandaliwa na Esther Macha kutoka Chunya mkoani Mbeya ,macha ni mwandishi wa gazeti la Majira mkoa wa Mbeya na mtandao wa chama cha waandishi wa habari za jinsia Tanzania (TGNP) mikoa ya kusini
Habari kwa Hisani ya Francis Godwin 


No comments: