Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, July 13, 2011

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 3 WA BARAZA LA WAKUU WA VYUO VIKUU HURIA AFRIKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa mkuu wa tatu wa Baraza la Wakuu wa Vyuo Vikuu huria Afrika wa siku tatu kuhusu Elimu ya mafunzo ya Masafa uliofunguliwa leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mhadhiri Chuo Kikuu Huria cha Zanzibar Tanzania, Grace Kissassi, wakati alipokutana naye baada ya kufungua rasmi mkutano mkuu wa 3 wa Baraza la wakuu wa Vyuo Vikuu huria kutoka Afrika, kuhusu elimu ya mafunzo ya masafa uliofunguliwa rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa 3 wa Baraza la Wakuu wa Vyuo Vikuu huria kutoka Afrika baada ya kuzindua mkutano huo kuhusu mafunzo ya Elimu ya Masafa.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo...
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa siku 3, kuhusu mafunzo ya Elimu ya Masafa unaowashirikisha wakuu wa Vyuo Vikuu Huria kutoka nchi za Afrika, uliofunguliwa leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
"

No comments: