Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT , Erwin Telemans, akiagana na mjumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza, Elizabeth Filkin, baada ya kumaliza ziara yake hospitalini hapo leo mchana (wapili kulia) ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa kampuni hiyo, Mwamvita Makamba, aliembatana na ujumbe huo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Haika Mawalla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw Erwin Telemans akimpatia maelezo Mjumbewa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Huduma kwa Jamii wa Vodafone ya nchini Uingereza, Elizabeth Filkin, wakiwa katika wodi ya wagonjwa wa mdomo sungura alipotembelea hospitalini hapo kuona maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Vodacom Foundation. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba, akimjulia hali mtoto mwenye tatizo la mdomo sungura. Elizabeth yupo nchini kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya kijamii inayofadhiliwa na Vodacom.
Mjumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza Elizabeth Filkin akipewa maelezo na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw. Erwin Telemans kuhusiana na wagonjwa wanaopata huduma katika Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam.
Muuguzi wa Hospital ya CCBRT kitengo cha wagonjwa wa Fistula Bi. Emelda Lweno akimwonyesha mjumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza Elizabeth Filkin wanawake wenye ugonjwa wa Fistula ambao matibabu yake yanafadhiliwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania wakati wa ziara yake hospitalini hapo.
Muuguzi wa Hospital wa Hospitali ya CCBRT kitengo cha wagonjwa wa Fistula, Emelda Lweno akitoa maelezo kuhusiana na jinsi wanavyowahudumia wagonjwa wa Fistula.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw. Erwin Telemans akifafanua jambo kwa mjumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza Elizabeth Filkin.Picha Na Muhidin Sufian
No comments:
Post a Comment