Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, June 13, 2011

WANANCHI KULIPA KODI KWA VODACOM M-PESA

Mkuu wa mauzo wa kitengo cha Vodacom m-pesa Franklin Bagalla kushoto akitoa maelezo kwa waandishi wa habari njia zinazotumika kulipia kodi kupitia huduma ya m-pesa ,katikati ni Naibu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Placidus Luoga,na Mkurugenzi wa Fedha TRA Saleh Mshoro ,Kampuni ya Vodacom kushirikiana na Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) jana imetanagza rasmi kuanza kutumika kwa njia hiyo ya m-pesa kulipia kodi.
Mkuu wa kitengo cha Mahusiano wa kampuni ya Vodacom Tanzania Nector Foya katikati akiwaonyesha Naibu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Placidus Luoga,na Mkuu wa kitengo cha Mauzo Vodacom m-pesa FranklinBagalla bango litakalotumika kuelimisha umma njia za ulipaji kodi kupitia huduma ya Vodacom m-pesa wakati wa utambulisho rasmi wa huduma hiyo kwa waandishi wa habari leo jijini dare s salaam.
Naibu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Placidus Luoga akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati wa utambulisho rasmi wa huduma ya malipo ya kodi kupitia Vodacom m-pesa inayotolewa na kampuni ya Vodacom Tanzania, kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa Mamlaka ya mapato Tanzania Saleh Mshoro na kushoto ni Mkuu wa Mauzo wa Vodacom m-pesa Franklin Bagalla.

No comments: