Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, June 13, 2011

*MAJAMBAZI YAPORA FEDHA HOSPITALI YA MUHIMBILI

Kundi la watu wanaodaiwa kuwa ni Majambazi wakiwa na Pikipiki wamevamia na kupora Mamilion ya fedha katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Tukio hilo la ujambazi limetokea leo asubuhi ambapo katika tukio hilo inadaiwa kuwa askari, Juma Magungu wa Kampunbi ya Full Time Security aliyekuwa zamu ya ulinzi katika Idara ya Uhasibu amepigwa risasi Kifuani na majambazi hao na kufariki dunia.
Habari zilizotolewa na Kituo cha Redio Uhuru Fm zimesema kuwa Ofisa uhusiano wa Hospitali hiyo, Ndugu Aminiel Aligeisha, alisema kuwa tukio hilo limetokea leo saa mbili asubuhi ambapo wahasibu wawili wa Hospitali hiyo walikuwa katika zoezi la kuhamisha fedha hizo kupeleka Idara kuu ya Uhasibu.
Wakiwa katika lilitokea kundi hilo la Majambazi kuwavamia na kisha kufanya tukio hilo na kutoweka.
Kwa mujibu wa Ofisa huyo, ni kwamba gari hilo lenye namba za usajili SU-36713 aina ya Nisani likiwa na watumishi wanne wa Idara hiyo walivamiwa na kundi hilo la majambazi wakiwa na Bastola moja.
Aidha alisema kuwa katika tukio hilo jumla ya Sh. milon 13 zinadaiwa kupotea.

No comments: