Mbunge wa Jimbo la Uzini Zanzibar na Mkurugenzi wa Zanzibar Media Corporation Seif Khatibu kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi bora wa kike wa nyimbo za asilia Sada Mohamed mara baada ya kumkabidhi tunzo yake kwenye Zanzibar Music Award,zilizofanyika juzi mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mjumbe wa NEC Aisha Kigoda kulia akimkabidhi Tunzo msani bora chipukizi wa kike Sauna G kwenye Zanzibar Music Award,zilizofanyika juzi mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mwanamziki wa kizazi kipya Baby J akiwa ameshikilia Tunzo yake aliyejinyakulia kwenye Zanzibar Music Award 2011, kuwa mwanamziki bora wa kike wa muziki wa kizazi kipya ,zilizofanyika juzi mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,kulia ni Hagai Samson aliyemkabidhi tunzo hiyo.
Meneja wa Vodacom Tanzania kanda ya Zanzibar Mohamed Mansour kulia akimkabidhi Tunzo Mwanamziki bora wa kiume wa nyimbo za kizazi kipya Juma Twenty kwenye Zanzibar Music Award,zilizofanyika juzi mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
No comments:
Post a Comment