Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, June 12, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA DKT ASHA MIGIRO NEW YORK


Hapa pia Dkt. Asha Rose Migiro, akimkabidhi zawadi, Makamu wa Rais, Dkt. Bilal.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha rose Migiro, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye Hoteli Intercontinental, alipofikia Makamu New York, jana Juni 10, 2011. Kushoto ni mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal.
Picha za pamoja na baadhi ya viongozi wa Tanzania waliohudhuria mkutano huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa nne kulia), mkewe Mama Zakhia Bilal (wa tatu kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha Rose Migiro (wa nne kulia) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim (wa pili kulia) na mbunge wa Viti Maalum (CCM) Lediana Mng’ong’o (kulia). Kutoka (kushoto) ni Balozi wa Tanzania wa Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue, Naibu Waziri wa Afya , Sawere Nkya, Waziri wa Afya wa SMZ, Juma Duni Haji na Waziri katika Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais SMZ, Fatma Fereji, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo baina ya Makamu wa Rais na Naibu Katibu Mkuu jana Juni 10, 2011, New York.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dkt. Asha Rose Migiro, wakati katibu huyo alipomtembelea jana Juni 10, 2011 na kufanya naye mazungumzo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dkt. Asha Rose Migiro, wakati katibu huyo alipomtembelea hotelini alikofikia jijini New York, jana Juni 10, 2011 na kufanya mazungumzo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, jijini New York jana Juni 10, 2011, kwa ajili ya kuhudhuria hatua ya ufungaji wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi, uliozishirikisha nchi zaidi ya 30.

No comments: