Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, June 1, 2011

Uzinduzi Wa Flaviana Matata Foundation Wafana Jijini Dar es Salaam

Mwanamitindo Flaviana Matata anayefanya kazi zake za uanamitindo katika jiji la New York nchini Marekani akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa Taasisi yake inayoitwa FLAVIANA MATATA FOUNDATION itakayokuwa ikisaidia na kusomesha watoto wa kike wasiokuwa na wazazi au walezi (Yatima). Taasisi hiyo ambayo itakuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakisaidia jamii hapa nchini akiwemo Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji, Mwamvita Makamba pamoja na wadau wengine. Uzinduzi huo umefanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu wakiwamo Wabunge, Wafanyabiashara wakubwa pamoja na Viongozi wa Serikali.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akieleza nia ya Flaviana Matata kuzindua Taasisi hiyo. Mwamvita Makamba ni mmoja wa wadau watakaokuwa wakisimamia taasisi hiyo pamoja wakishirikiana na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Clouds FM Ruge Mutahaba.
Bi. Teddy Mapunda akifurahi jambo na Mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha CLOUDS FM Gerarld Hando katika hafla fupi ya uzinduzi wa FLAVIANA MATATA FOUNDATION.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akieleza nia ya Flaviana Matata kuzindua Taasisi hiyo. Mwamvita Makamba ni mmoja wa wadau watakaokuwa wakisimamia taasisi hiyo pamoja wakishirikiana na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Clouds FM Ruge Mutahaba.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Mwansoko akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Fenela Mkangara wakati wa uzinduzi wa FLAVIANA MATATA FOUNDATION ambapo alimpongeza kwa kuonyesha kujali maendeleo ya mtoto wa kike hapa nchini na kuahidi kushirikiana naye bega kwa bega.
Mh. Mohammed Dewji (katikati) katika tete atete na Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL Bi.Teddy Mapunda pamoja na Mkurugenzi wa Masoko MULTICHOICE Tanzania Bi. Furaha Sumalu.
Operation Manager wa MULTICHOICE Tanzania Ronald Baraka Shelukindo pamoja na Marketing Manager wa DT DOBIE Tanzania Alfred Minja (kulia).
Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL Bi.Teddy Mapunda akibadilishana mawazo na Mtangazaji wa Radio Choice FM Babbie Kabae ambaye alikuwa ni mshereheshaji (MC) katika hafla hiyo.
Picha zote na Mdau Zainul na John Bukuku


No comments: