Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, June 1, 2011

Alichokifanya Nape Nnauye Mwingulku Rukwa

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga, jana, siku ya kwanza ya ziara yake na Mjumbe wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, mkoani Rukwa
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa CCM, Theresia Mwanakatwe, katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi, jana katika mji mdogo wa Laela, wilayani mkoani Rukwa. Jumla ya wanachama wapya 82, waliojiunga na CCM walikabidhiwa kadi. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Nchemba Mwigulu.
KATIBU wa NEC, Uchumi na Fedha CCM, Nchemba Mwigulu akikabidhi kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kadi za wanachama kutoka vyama vya upinzani ambazo wanachama wa vyama hivyo walimkabidhi baada ya kutangaza kuhama vyama vyao na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana, katika Uwanja wa Mandela, mjini Sumbawanga. Mbali na CUF na NCCR-Mageuzi, Chadema pekee walihama 51.
Nape akiteta jambo na Mbunge wa zamani wa Nkwela Crisant Mzindakaya
Watoto na vijana wakimzunguka Nape baada ya mkutano katika mji mdogo wa Laela
MKAZI wa kijiji cha Ntendo, Zakaria Lusambo akimshukuru, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye baada ya kukabidhiwa baiskeli ya miguu mitatu pamoja na wenzake wanne wenye ulemavu wa miguu, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jana, kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga. Baiskeli hizo zimetolewa na Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hilary (kushoto)
Napa akishiriki kucheza ngoma na kina mama wa Laela
Habari kwa hisani ya Haki Ngowi Blog

No comments: