Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, June 12, 2011

SIMBA YAICHAPA MOTEMA PEMBE GOLI 1-0 U/TAIFA

Mchezaji wa timu ya Simba Mussa Hassan Mgosi akiwa amembeba mchezaji mwenzake Amri Kiemba mara baada ya kupachika goli la kwanza na la ushindi, katika goli la timu ya Motema Pembe kutoka DRC kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF, uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii, goli hilo limefungwa kipindi cha kwanza dakika ya 20 ya mchezo huo mshabuliaji Mgosi aliipokea pasi nzuri kutoka kwa kiungo Mohamed Banka kufunga goli hilo pekee, hivyo Simba imefanikiwa kuwatoa 'ulimi nje' wapinzani wao Motema Pembe ya DRC.
Mchezaji Emmanuel Okwi akimtoka beki wa timu ya Motema Pembe katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la CAF katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mshika kibendera akiangalia wakati wachezaji wa timu ya Simba na Motema Pembe wakichuana katika mchezo wao unaofanyika sasa kwenye uwanja wa Taifa
Mashabiki wa timu ya Simba wakiangalia mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.(picha kwa hisani ya FULL SHANGWE Blog)

No comments: