Hili ni bwawa kubwa la maji ambalo lipo katika bara bara ndani ya Mabibo Hostel za Chuo kikuu cha mlimani
Muda wa sa Moja na nusu usiku wanafunzi wa Mabibo Hostel wakiwa wanakwepa Njia hiyo yenye Madimbwi makubwa na kukanyaga viunga vya mauwa ikiwa ndio njia mpya waliyo igundua baada ya njia yao kuharibiwa vibaya na wahusika kupaangalia bila kufanya jambo lolote.
Hii ndio kero kubwa pale Mabibo Hostel za Chuo kikuu cha Mlimani Jijini Dar es salaam ambapo wanafunzi wamelalamika sana eneo hilo lifanyiwe ukarabati lakini watu wahusika wamefumbia macho na kuziba masikio hali inayo sababisha usumbufu na kero kubwa wakati wa mvua kwa bara bara hiyo iliyo chimbika vibaya. Wanafunzi hao wameomba wahusika kulifuatilia swala hilo mapema kwa sababu licha ya kusababisha foleni ya kupishana wakati wote hasa usiku lakini pia inasababisha magari madogo kukwama eneo hilo husika. Hatukubahatika kuwahoji wanafunzi lakin hivi karibuni mtawasikia wanafunzi wanasemaje juu ya kero hii.
No comments:
Post a Comment