Ilikuwa siku ya Jumamosi ambapo Kamera yetu ilikua vijijini kama kawaida na kumkuta kijana Amosi live akiwa anatokea mtoni kufua nguo zake za shule na za kushindia.
Nilipo jaribu kumuhoji baadhi ya maswali alisema kuwa, "Mimi napendelea sana kufanya usafi siku za juma mosi ukizingatia kuwa ndio siku napata muda, kwa maana nakuwa bize na shule asubuhi nikiludi mchana kuchunga Ng'ombe,kondoo na mbuzi usiku kusoma kwa hiyo leo ndio nimepata muda wa kufua" Hata hivyo kijana huyo hakuongea tena akaenda zake kama anavyo onekana hapa.
Sikubaki nyuma niliendelea kumfutilia kwa ukaribu zaidi ingawa alinipotea kidogo, Baada ya muda kidogo nikakuta ametua mzigo wake eneo hili la kijani kibichi iliapate kuanika pamba zake.
Huu ni mwendelezo tuu wa kamera yetu vijijini.
No comments:
Post a Comment