Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na mashirika mengine imedhamini mpango wa kipekee wa kuwaongezea morali wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini ili kuwawezesha kuwa tayari kimaisha mara watakapohitimu masomo yao.
Katika mpango huo ulioandaliwa na kitengo cha huduma kwa jamii cha kampuni ya East Africa Speakers Bureau (EASB) cha jijini Dar es Salaam Vodacom Tanzania uliozinduliwa Chuo cha Uandishi wa Habari (SJMC) Vodacom Tanzania imedhamini kwa milioni 38/-.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Afisa bidhaa na huduma wa Vodacom Tanzania Elihuruma Ngowi alisema fedha zlizotolewa na kampuni yake zitawezesha wanafunzi kupata ujuzi na mbinu zitakazowajenga katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na kukuza na kufanikisha shughuli za ujasiriamali.
Ngowi alitaja mafanikio mengine kuwa ni kujipatia ujuzi wa kuwa na mbinu za mikakati fanisi kwa ajili ya kufikia malengo yao ya kibiashara na kwamba mbinu hizo watakazozipata pia zitatumika kwa manufaa yao na taifa kwa ujuamla.z
“Tunafurahi kuwa sehemu ya kusanyiko hili ambalo linajumuisha wanafunzi kutoka mikoa tofauti yenye tamaduni mbalimbali ambao kwa pamoja watachangia mbinu watakazozitumia baada ya kumaliza masomo yao,” alisema Afia huyo wa huduma wa Vodacom Tanzania.
Kwa upande wake Rais wa EASB Paul Mashauri alisema maudhui ya mafunzo hayo yatakuwa changamoto na yatawawezesha wanafunzi kuibua naswali yanayotokana na somo husika ili kuinua uelewa wa mikakati mbalimbali ya biashara.
Alisema mpango huo utakuwa na sehemu mbili za mafunzo ambapo ya kwanza inayoanza April mwaka huu itahusisha shindano la chemsha bongo kuhusu umuhimu wa kuitambua sekta binafsi kwa ajili ya mustakabali ujao wa nchi na kizazi chote kwa ujumla.
“Kusoma na kutenda ni vitu viwili tofauti, kuna vitu vipo mtaani lakini havifundishwi vyuoni, hivyo ukikutana na watu mnaweza kukaa na kujadili kwa pamoja ili kupanua uelewa utakaowezesha kufikia malengo mliojiwekea kimaisha,” alisema Mashauri.
Nae mwanachuo wa SMJC Monica John alisema mpango huo umekuja katika muda muafaka kwani wanafunzi wengi baada ya kuhitimu mafunzo yao wanashindwa kujiajili kwa kukosa uelewa na badala yake hutegemea ajira kutoka serikalini au kwenye taasisi binafsi.
“Mafunzo haya ya kutujengea uwezo tunayopatiwa ni wazi yatatujenga kuweza kujiamini na kujiendesha kimaisha mara tutakapomaliza chuo na binafsi napenda kuwashukuru waliofikiria kuuleta mpango huu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini,” alisema Monica.
Vyuo vitakavyoshiriki ni Chuo cha Ardhi, CBE, DUCE, UDOM, IFM, Chuo cha Ustawi wa
No comments:
Post a Comment