Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers
Network' – TBN inawaomba wanachama wake wote kutotumia taarifa ama
habari au picha yoyote kutoka katika mkutano wa maadhimisho ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari (WPFD) unaofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Kamati
Kuu ya Uongozi TBN imefikia hatua hiyo leo baada ya kujadiliana na
kujiridhisha kuwa kumekuwepo na taasisi za tasnia ya habari ambazo
zimekuwa zikiwatenga wanahabari wa mitandao ya kijamii (bloggers) na
kutotambua umuhimu wao wakati sehemu kubwa ya taarifa mbalimbali nchini
husambazwa na mitandao hiyo.
TBN
iliyosajiliwa rasmi serikalini Aprili 2015 na kupewa namba ya usajili;
S. A 20008 inawataka wanachama wake kutotoa ushirikiano wa sina yoyote
kwa taasisi ambazo zinawatenga bloggers.
Tunasikitika
kufikia hatua hii ila hamna jinsi. TBN itasikitika na kumshangaa
mwanachama wake au blogger asiye mwanachama kutounga mkono agizo hili,
na kwenda kinyume na agizo hili. Muda umefika ‘Bloggers’ kudai heshima,
kutambulika na kuthaminika kama tasnia ya habari ingine yoyote.
Imetolewa na;-
Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim E. Mushi
03/05/2016
No comments:
Post a Comment