Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na wadau wa zao la Kahawa kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe na Katavi kuhusu changamoto za zao hilo |
wadau wa zao la Kahawa kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe na Katavi wakijadiliana mbinu na changamoto mbali mbali zinazowakabili. |
MKUU
wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewataka Maofisa Ugani kutojibweteka maofisini
na kuhesabu mafaili na badala yake waende mashambani kutoa ushauri wa kilimo
bora na matumizi ya pembejeo.
Akizungumza
na wadau wa zao la Kahawa kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe na Katavi, Makalla
alisema, maofisa Ugani wanabaki maofisini ilhali shughuli za kilimo zipo
mashambani hali inayosababisha wakulima kuendelea kulima bila kupata ushauri
kutoka kwa wataalamu.
‘’Ondokeni
maofisini wafuateni wakulima mashambani,huko mtakutana na changamoto nyingi
zinazosababisha kupungua kwa uzalishaji wa zao la Kahawa.’’ Alisema.
Aidha waliwataka wakulima wa zao hilo kuzingatia ushauri unaotolewa na taasisi ya utafiti wa zao hilo TaCRi ili kuongeza tija ya uzalishaji wa kahawa.
No comments:
Post a Comment