Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, May 8, 2016

RC MBEYA AWATAKA MAOFISA KILIMO KWENDA MASHAMBANI




Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na wadau wa zao la Kahawa kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe na Katavi kuhusu changamoto za zao hilo

wadau wa zao la Kahawa kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe na Katavi wakijadiliana mbinu na changamoto mbali mbali zinazowakabili.

MKUU wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewataka Maofisa Ugani kutojibweteka maofisini na kuhesabu mafaili na badala yake waende mashambani kutoa ushauri wa kilimo bora na matumizi ya pembejeo.

Akizungumza na wadau wa zao la Kahawa kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe na Katavi, Makalla alisema, maofisa Ugani wanabaki maofisini ilhali shughuli za kilimo zipo mashambani hali inayosababisha wakulima kuendelea kulima bila kupata ushauri kutoka kwa wataalamu.

‘’Ondokeni maofisini wafuateni wakulima mashambani,huko mtakutana na changamoto nyingi zinazosababisha kupungua kwa uzalishaji wa zao la Kahawa.’’ Alisema.

Aidha waliwataka wakulima wa zao hilo kuzingatia ushauri unaotolewa na taasisi ya utafiti wa zao hilo TaCRi ili kuongeza tija ya uzalishaji wa kahawa.

No comments: