Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, May 8, 2016

RC MBEYA AWAALIKA WADAU KUSAIDIA MICHEZO MKOANI MBEYA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akitoa neno la shukrani kwa Coca cola Kwanza kwa kudhamini michezo ya UMISETA.


Afisa Masoko wa Cocacola akitoa neno na shukrani kwa viongozi waliofika kwenye uzinduzi wa mashindano ya Copa Cola Kwanza kwa kushirikiana na UMISETA Mkoa wa Mbeya  kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya.


Ofisa Masoko Msaidizi wa Coca Cola Kwanza, Mariam Sezinga akizungumza jambo.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akijiandaa kupiga mpira kulenga goli kuashiria uzinduzi wa mashindano ya michezo ya Copa Cola Kwanza kwa kushirikiana na UMISETA  Mkoa wa Mbeya  katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akipiga mpira kulenga goli kuashiria uzinduzi wa mashindano ya michezo ya Copa Cola Kwanza kwa kushirikiana na UMISETA  Mkoa wa Mbeya  katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (katikati) akikabidhi vifaa vya michezo kwa wanafunzi  wa Shule ya Sekondari Forest ya Jijini Mbeya  kwa niaba ya Shule zote za Jiji la Mbeya ambazo zinashiriki mashindano ya Copa Coca Cola kwanza kwa kushirikiana na UMISETA Mkoa wa Mbeya kwenye uzinduzi wa mashindano hayo katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Vifaa hivyo vilitolewa na Coca Cola Kwanza.

Wanafunzi wa Shule mbali mbali za Sekoandari jijini  Mbeya,  wakishangilia wakati wa michezo ikiendelea ndani ya Uwanja wa Sokoine Jijini hapa kwenye uzinduzi wa michezo ya UMISETA wanayoshirikiana na Copa Cola Kwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akimkabidhi vifaa vya michezo mmoja wa Wanafunzi wa Sekondari Mkoa wa Mbeya kwa ajilin ya mashindano


Baadhi ya Wanafunzi kutoka shule mbali mbali wakishuhudia zoezi la kukabidhiwa vifaa vya michezo

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewaalika wafadhili na wadau mbalimbali mkoani humo kuchangia michezo ili kuimarisha afya, mwili na akili.

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa vya michezo kwa shule za sekondari mkoani Mbeya(UMISETA) Makalla alisema wanafunzi wanahitaji sapoti kubwa katika kuimarisha michezo ili kuwajengea mustakabali mzuri na kuimarisha vipaji vyao.

Aliwapongeza Kampuni ya vinywaji baridi ya Cocacola ambao wameonesha njia kwa kufadhili vifaa vya michezo kwa ajili ya michezo ya UMISETA hali ambayo itaendelea kuimarisha ari na nguvu wa vijana kupenda michezo nchini.

No comments: