Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, May 23, 2016

NMB YAZINDUA MTANDAO WA WATEJA WAKUBWA

Afisa Mkuu wa Wateja wakubwa na serikali – Richard Makungwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa NMB Executive Network uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. NMB iliandaa mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara na wateja wakubwa wa benki hiyo wanaotoka kanda ya Nyanda za juu wenye mzunguko wa mitaji usiopungua shilingi Bilioni 10. Zaidi ya wateja 100 walihudhuria ambapo pamoja na mambo mengine, walipewa mafunzo na kujadiliana jinsi ya kukuza mahusiano ya kibiashara yenye tija kati ya benki na wateja wake. 



Afisa Mkuu wa Wateja wakubwa na serikali – Richard Makungwa akimkabidhi kadi maalumu ya uanachama wa wateja wakubwa (NMB Executive Network) Lightness Ndelwa anayemiliki duka la lightness Fashions katika mkutano uliofanyika jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. NMB iliandaa mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara na wateja wakubwa wa benki hiyo wanaotoka kanda ya nyanda za juu na wenye mzunguko wa mitaji usiopungua shilingi Bilioni 10. Zaidi ya wateja 100 walihudhuria ambapo pamoja na mambo mengine walijadiliana jinsi ya kukuza mahusiano ya kibiashara yenye tija kati ya benki na wateja wake. Katikati ni Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Badru Idd.

Afisa Mkuu wa Wateja wakubwa na serikali – Richard Makungwa akimkabidhi kadi maalumu ya uanachama wa wateja wakubwa (NMB Executive Network membership) Mfanyabiashara wa Simu jijini Mbeya –Esther Mbogela. NMB iliandaa mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara na wateja wakubwa wa benki hiyo wanaotoka kanda ya nyanda za juu na wenye mzunguko wa mitaji usiopungua shilingi Bilioni 10. Zaidi ya wateja 100 walihudhuria ambapo pamoja na mambo mengine walijadiliana jinsi ya kukuza mahusiano ya kibiashara yenye tija kati ya benki na wateja wake. Katikati ni Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Badru Idd.

Afisa Mkuu wa Wateja wakubwa na serikali – Richard Makungwa akimkabidhi kadi maalumu ya uanachama wa wateja wakubwa (NMB Executive Network membership) Mfanyabiashara maarufu wa mbao jijini Mbeya - Bi Esther Mbilinyi katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. NMB iliandaa mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara na wateja wakubwa wa benki hiyo wanaotoka kanda ya nyanda za juu na wenye mzunguko wa mitaji usiopungua shilingi Bilioni 10. Zaidi ya wateja 100 walihudhuria ambapo pamoja na mambo mengine walijadiliana jinsi ya kukuza mahusiano ya kibiashara yenye tija kati ya benki na wateja wake. Katikati ni Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Badru Idd.
 

 NMB Executive Network (NEN) Ni mtandao wa wateja wakubwa na wanaochipukia wenye mzunguko wa fedha kuanzia shilingi Bilioni 10 kwa mwaka. Tunawakaribisha pia wateja na wasio wateja wa NMB kwaajili ya kuwaonyesha fursa na bidhaa za NMB.
                                                                        

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mtandao huo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mbeya, Afisa Mkuu wa Wateja wakubwa na serikali, Richard Makungwa alisema  Mpango huu ulianza mwaka 2014 huku ukilenga miji mikubwa 6 nchini yaani Dar es Salaam , Mwanza, Mbeya, Morogoro, Arusha and Kilimanjaro.


Alisema Mpaka sasa, mtandao huu upo kwenye mikoa mitano tu ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Morogoro.


Alisema kwa Mkoa wa Kilimanjaro (Moshi), mtandao huu upo mbioni kuzinduliwa na utazinduliwa sambamba na  Kituo kipya cha biashara cha NMB (New Business Center) ambapo mpaka sasa, tuna washirika 286  wa mtandao wa NMB Executive Network.


Makungwa alisema Makusudi makubwa ya kuanzisha mtandao huu ni kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya benki na wateja wake na kuweka mahusiano yenye tija kwa pande zote mbili yaani kwa mteja na kwa upande wa benki huku tukiangazia wateja wakubwa tu.


Alizitaja faida za mtandao huo kuwa ni pamoja na Uwezeshaji kimaarifa (Elimu juu ya mipangilio ya Biashara, elimu ya kodi pamoja na taratibu mbalimbali za serikali juu ya biashara).


Faida nyingine ni wateja  kupata Fursa ya kukutana na uongozi wa juu wa benki pamoja na menejimenti na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi, Fursa ya kukutana  na wafanyabiashara mbalimbali na kubadirishana mawazo,Fursa ya kutoa mapendekezo juu ya bidhaa za NMB, Fursa ya kutoa mrejesho wa huduma za kibenki za NMB.


Alizitaja faida zingine kuwa ni Kupata upendeleo kwa kupewa kadi maalumu za uanachama zinazokupa upendeleo wa huduma unapotembelea matawi yetu nchi nzima,Kupata upendeleo wa bei ya kubadirisha fedha za kigeni.



No comments: