Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa Mariam Mtunguja alipokutana na wanahabari wa mkoa wa Mbeya |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Mbeya kwenye ukumbi wa Mkapa |
Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa TAJATI Felix Mwakyembe akizungumza jambo mbele ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla kwenye ukumbi wa Mkapa |
Makamu Mwenyekiti wa TAJATI Christopher Nyenyembe akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla kwenye ukumbi wa Mkapa |
MKUU
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewataka waandishi wa habari kuandika habari zilizofanyiwa utafiti na kweli zenye changamoto ili kuleta tija kwa
jamii.
Makalla
alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki katika kikao chake cha kujitambulisha kwa
waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa Mkapa uliopo jijini hapa.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema ni vema Waandishi wa habari wakajilita katika kuibua
habari za kweli na zenye changamoto zitakazoisadia serikali kuongoza na kutatua
kero zinazoikabili jamii kwa ujumla.
Mbali
na kutoa wito huo, Makalla aliomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa waandishi
wa habari ili aweze kufanya kazi tofauti na mategemeo ya wengine wanaodhani
anafanya siasa.
‘’Nataka
wanasiasa wajue kuwa mie sifanyi siasa bali nimekuja kufanya kazi, najua wazi
kuwa Jiji la Mbeya na halmashauri yake iko chini ya upinzani,wanasiasa wafanye
siasa zao mie ninafanya kazi naomba ushirikiano wenu Waandishi,’’alisema Mkuu
wa Mkoa.
Aliongeza
kuwa uwezo wake wa kufanya kazi kwa kujituma na kutimiza wajibu wake unatokana
na malezi mazuri aliyoyapata kutoka kwa wazazi wake ambao walimuusia kufanya
kazi kwa bidii kupita malengo.
Alisema
wapo baadhi ya wanasiasa wanabeza uongozi wake pamoja na utendaji kazi wake
wakihusisha na mambo ya siasa ingawa
baadhi ya wanasiasa wanadhani utendaji wake unashinikizwa na kasi za kisiasa.
‘’Mie
ni mtoto niliyekulia kwenye line za polisi, baba yangu na mama yangu walikuwa
ni askari polisi, wote wameshatangulia mbele ya haki, Baba yangu aliniusia
Nikipewa kazi nifanye kikweli kweli, na kiukweli ninapopewa kazi nafanya kazi
kila nilipopewa majukumu huwa natimiza wajibu wangu i am serious nimekuja
kufanya kazi sio siasa,’’alisisitiza.
Sanjari
na azma yake hiyo ya kufanya kazi pia amewataka wanahabari kushiriki katika
kuibua changamoto zilizopo ili ziweze kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Mbeya
katika nyanja za kiuchumi na kijamii.
Alisema
wanahabari ni sekta muhimu inayoweza kuisaidia serikali katika kuibua mambo ya
msingi ambayo yanaweza kuchukuliwa na kufanyiwa kazi na serikali.
Aidha
Makalla ameelezea changamoto mbalimbali za utendaji zilizopo kwa watumishi wa
umma huku akiweka bayana tatizo la watumishi hewa ambalo limeisababishia hasara
serikali na kuwa amedhamiria kurejesha dhana ya utumishi bora kwa watumishi wa
umma.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya, Modest
Nkulu alitoa wito kwa uongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kujiepusha na
vitendo vya kuwagawa waandishi hususani katika ziara mbali mbali.
Alisema
ni kawaida viongozi wa Mkoa kubagua baadhi ya vyombo na waandishi jambo ambalo
husababisha umoja wa waandishi kugawanyika na kukosa ushirikiano.
No comments:
Post a Comment