Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, March 31, 2016

WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZA UJARANI MWEMA.

Mkuu wa Wilaya ya Karonga nchini Malawi,Rosemary Moyo(aliyesimama) akizungumza jambo katika kikao cha ujirani mwema huku Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dk.Thea Ntara akimsikiliza kwa makini.Baadhi ya wajumbe wa kikao cha ujirani mwema kati ya Wilaya ya Karonga na Wilaya ya Kyela wakifuatilia mjadala unaoendeleaILI kuimarisha ujirani mwema kati ya Wilaya ya Kyela na Karonga ya Nchi jirani ya Malawi, Wilaya hizo zimekutana katika kikao cha pamoja ili kujadili changamoto zinazowakabili.

Kikao hicho cha ujirani mwema kilifanyika juzi katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kwa ajili ya kujadili changamoto zinazozikabili Wilaya hizo.

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na  Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dk. Thea Ntara aliyewakilisha upande wa Tanzania na kwa upande wa Wilaya ya Karonga iliwakilishwa na Rosemary Moyo ambapo baadhi ya changamoto kubwa zinazozikabili Wilaya hizo na kujadiliwa kuwa ni pamoja na wahamiaji haramu,madawa ya kulevya,pombe kali na wizi wa pikipiki.

Wakizungumza katika kikao hicho, Baadhi ya wajumbe kutoka pande zote mbili walisema  tatizo la wahamiaji haramu kutoka nchi za Ethiopia,Somalia,Congo,Burundi,Rwanda na Nigeria kunachangiwa na ukosefu wa umakini kutoka mipaka ya kaskazini ambapo huwaacha wahamiaji hao kuingia kiholela.

Walisema sababu nyingine inachangiwa na baadhi ya watumishi wa umma wa pande hizo mbili   kutodhibiti vitendo hivyo kutokana wa baadhi ya wahamiaji kutumia pesa pindi wanapokamatwa na baadhi ya maafisa usalama wasio waaminifu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karonga, Rosemary Moyo alisema kuwa Watanzania na Wamalawi ni ndugu wa damu ambao wametenganishwa na wakoloni kwa njia ya mpaka wa mto Songwe kwani mpaka sasa raia wa mpakani huvuka kutembeleana kila siku na wengi wao wameoleana kutoka pande hizo mbili.

Alisema  kutokana na tatizo hilo kubwa kwa nchi hizo Serkali zote huingia gharama kubwa kuwatunza na kuwasafirisha wahamiaji haramu  kuwarejesha nchi walizotoka.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dk. Thea Ntara alisema Wilaya ya Kyela imeimarisha ulinzi mpakani kwa kushirikiana na wananchi ndiyo maana wamefanikiwa kukamata wahamiaji wengi haramu waliojaribu kuvuka mpaka kupitia wilaya hiyo hivyo juhudi kubwa zifanyike ili kuhakikisha tatizo hilo linakomeshwa kabisa.

Aliongeza kuwa  elimu itolewe kwa raia wa pande zote mbili ili watu wanaowatilia shaka watolewe taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hizo mbili.


No comments: