Meneja Mkazi wa Kampuni ya Smile Tanzania Bw. Erick Bahner Akizungumza na Waandishi wa Habari ambao (Hawapo Pichani)
Katika harakati za
kuhakikisha wateja wake nawatanzaniakwa Ujumla wanafikiwa na huduma mtandaoni zenye
ubora wa hali ya juu, kampuni ya Smile Tanzania imetengeneza historia nyengine nchini wa uzunduzi wa huduma mbili zinazotumia
mtandao wa intaneti wa 4G LTE.
Akizungumzia juu ya uvumbuzi huo katika huduma za intaneti
Meneja Mkazi wa kampuni ya Smile nchini, Bw. Eric Behner,ameeleza kuwa huduma
hizoni SmileVoice inayowawezesha wateja kupiga simu mtandaoni ambayo ni ya
kwanza nchini yenye kusikika kwa ubora mkubwa na SmileUnlimited ambayo inatoa
fursa kwa mteja kutumia huduma ya intaneti bila kikomo ndani ya siku 30.
SmileVoice ni huduma ya hali ya juu inayopatikana kwenye
vifaa vya Android na Apple iPhone kupitia app na kumwezesha wateja kupiga simu
mtandaoni ikitumia huduma ya Smile 4G LTE na kumpa mteja uwezekano wa
SuperClear voice yaani High definition.
“Smile ni kampuni ya kwanza ya huduma za mawasiliano ya
simu duniani kuanzisha na kuendelezaprogramu ya bure ya huduma ya kupiga simu
mtandao wa 4G LTE kutumia app. Huduma hiiinawawezesha wateja wetu nchiniTanzania
wenye simu za Android na iPhone kufurahia kupiga simu zenye ubora wa hali ya
juu kupitia intaneti yetu yenye kasi zaidi. Tumejizatiti kwa kiasi kikubwa
katika kuhakikisha tunaboresha huduma za kupiga simu na mtandao wa intaneti.
Kwa kupitia huduma ya Smile Voice, wateja wetu wanaweza kupiga simu nchinina
nje ya nchi kama mitandao mingine ya simu.” Alisema Bw. Behner
“Mbali na huduma ya Smile Voice, Smile, kupitia kukusanya
rasilimali za kutosha, Smile imefanikiwa kutanua huduma zake mtandao wa 4G LTE mpaka kufikia miji 7 nchini Tanzania na sasa kuwapa fursa wateja kutumia intaneti
bila kikomo ndani ya siku 30 yenye kasi zaidi. Hakuna kampuni nyingine
nchiniinayotoa huduma kamahiyo zaidi ya Smile.” Aliongezea Bw. Behner
Akifafanua zaidi kuhusu huduma ya Smile Unlimited, Bw.
Behner amesema kuwa huduma hiyo ipo ndani ya sera ya kampuni ya usawa katika
matumizi. Sera hii itamfaidisha mteja kwani itamuhakikishia kuwa anakuwa ameunganishwa
kwa uhakika ndani ya sikuzote 30.
Programu ya SmileVoice app inawawezesha wateja ambao
hawanasimu za VOLTE uhakika wakupiga simu kupitia mfumo wa LTE
wakiwawameunganishwa na mtandao wa intaneti wa Smile.
“Katika soko la Tanzania, watu wenye vifaa vinavyotumia
Android ndivyo vinavyo ongoza na ukijumlisha na SmileVoice app, basi
tunawahakikishia wateja wetu watakaosajili nasi watajionea na kujivunia upigaji simu zenye ubora wa hali ya juu
kupitia simu zao.” Aliongezea Bw. Behner
Ili kuweza kutumia huduma ya Smile Voice,inambidi mteja
awe na SIM iliyosajiliwana akiwa na kifurushi cha Smile. Programu hii inaweza kupakuliwa
(downloaded) kwenye simu zinazotumia mfumowa Android na za iPhone (IOS) na
hufanyakazi mara tubaada ya mteja kujisajilinayo mara moja.
Wakati simu
ikiwahaina intaneti ya mtandao wa Smile mteja anaweza kupiga simu kwenda simu
nyingine ambayo imeunganishwa na mtandao wa intaneti wa 3G, Wi – Fi au nje ya
nchi.
Kwa
Masiliano zaidi;
Linda Chiza
Smile
Communications Tanzania
SmileVoice
number: +255 662 222 221
Mobile:
+255 758 811280
Email:
linda.chiza@smilecoms.com
On behalf of:
Smile
Communications Tanzania Ltd
www.smile.co.tz
No comments:
Post a Comment