Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, March 10, 2016

TCRA KUZIMA SIMU FEKI USIKU WA JUNI 30,2016.

 
Naibu mkurugenzi wa huduma kwa watumiaji bidhaa za mawasiliano wa  Thadayo Ringo akionesha simu feki inavyofanana na simu halali.
            Mhandisi mfumo Rajisi Imelda Salum akifundisha namna ya kutofautisha simu feki
                                  Eng: Lilian Mwangoka akifafanua jambo kwa waandishi

Baadhi ya waandishi wakisikiliza kwa makini maelezo ya viongozi wa mamlaka ya mawasiliano TCRA
   Mwandishi wa gazeti la Uhuru Solomoni Mwansele akitazama kwa makini kuibaini simu feki
        Katibu Mkuu wa Chama cha waandishi wa habari za  Utalii na Uwekezaji Tanzania TAJATI Venance Matinya akiuliza swali
                                       Mwandishi wa habari gazeti la Majira Rashidi Mkwinda akiuliza swali
                                                 Mwandishi wa habari Star Tv Amina Saidi akiomba ufafanuzi
                              Mwandishi wa Habari gazeti la Mwananchi Brand Nelson akiomba mwongozo wa jambo fulani
                                                   Naibu katibu Mkuu TAJATI Patrick Kosima akiuliza swali.

                                             
ILI kudhibiti vifaa vya mawasiliano visivyokuwa na ubora kwa mtumiaji, Wananchi wametakiwa kujenga utamaduni wa kudai risiti pindi anaponunua na kuhakikisha muuzaji anatoa muda wa garantii usiopungua miezi kumi na mbili kwa kifaa alichouza.
 
Wito huo ulitolewa jana na Naibu Mkurugenzi wa huduma za mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano,(TCRA)Thadayo Ringo,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani nchini(CEIR) katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za TCRA Kanda ya Nyanda za juu kusini jijini Mbeya.
 
Ringo alisema Mamlaka hiyo imejipanga kuanza kuzima simu za kiganjani ambazo ni feki usiku wa saa sita mwezi Juni mwaka huu hivyo ili kuepuka na kuzimiwa Simu ni vema wateja wakawa na utaratibu wa kudai risiti na kupewa muda wa garantii ili ikizimwa iwe rahisi kuirudisha kwa muuzaji.
 
Alisema mbali na mteja kudai risiti na kupewa muda wa garantii usiopungua miezi 12 utamsaidia mwananchi kurudisha simu au kifaa cha mawasiliano endapo kitakuwa kimeharibika kabala ya muda huo nay eye kutengenezewa ama kubadilishiwa bidhaa nyingine.
 
Aliongeza kuwa kupitia mfumo huo utairahisishia mamlaka kumbaini muingizaji wa bidhaa zisizokuwa na ubora kutokana na kufuatilia mlolongo mzima wa muuzaji hadi kumpata mwagizaji ili aweze kudhibitiwa kwa mujibu wa sheria.
 
Mkurugenzi huyo alisema kupitia mfumo wa rajisi ambao utakuwa na njia tatu ambazo ni orodha ya namba tambulishi ambazo vifaa vyake vinaruhusiwa, orodha ya namba tambulishi ambazo hutolewa  kuwa zimefungiwa na namba tambulishi ambazo zimefungiwa kwa muda au kuruhusiwa kwa muda utasaidia kurahisisha huduma za mawasiliano.
 
Alizitaja faida za mfumo wa rajisi ya namba tambulishi kuwa utasaidia kudhibiti wizi wa simu ambapo mtu aliyeibiwa ama kupoteza simu anaweza kutoa taarifa kwenye mamlaka na kasha kuifunga ili isifanye kazi tena.
 
Alisema faida nyingine ya mfumo huo utasaidia kuhimiza utii wa sheria kwa mujibu wa kifungu cha 128 cha EPOCA ambacho kinamtaka mtumiaji wa simu kutoa taarifa ya kupotea kwa simu au laini sambamba na kampuni ya simu kutokutoa huduma kwa simu iliyofungiwa.
 
Alisema faida nyinine ni kujenga misingi ya matumizi ya simu halisi zisizo bandia ambapo mtumiaji ataweza kutambua iwapo simu aliyonayo inakidhi viwango na ni halisi sio bandia kwa kubonyeza alama zilizowekwa na mamlaka.
 
“Mmiliki wa simu anapiga nyota reli sifuri  sita kasha reli anapata namba zake za utambulisho yaani Imei ambazo anazituma kwenda 15090 hapo analetewa maelezo kuwa simu anayotumia inaoana kati ya kampuni iliyotengeneza na imei namba” alifafanua Naibu Mkurugenzi.
 

No comments: