Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, March 9, 2016

AWASHUKURU WALIOSHIRIKI MAZISHI YA MWANAE

Jeneza lenye mwili wa marehemu Negro Award Mpandila ukiwa kanisani kwa ajili ya sala ya mwisho

Wanafamilia na waombolezaji wakiwa kanisani

Ibada ya kumsindikiza marehemu ilifanyika katika kanisa la Sabato Dar es salaam na Mbeya

Ndugu Jamaa na marafiki wakiwa katika sura za huzuni

Ndugu wa marehemu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kuzika





Marafiki kutoka Hospitali ya Mkoa wa Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja na wafiwa

FAMILIA ya ndugu Award Mpandila inawashukuru wananchi wote kwa ujumla kwa kushiri kwa namna moja au nyingine katika kuwafariji na kuwasaidia katika kipindi ambacho familia hiyo imempoteza  mtoto wao mpendwa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa Award Mpandila alisema anawashukuru watu wote walishiriki kuanzia kuaga mwili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuungana nao katika mazishi yaliyofanyika kijijini Ntokela Mkoa wa Mbeya jana.

“Asante Ndugu zangu wote mnaozidi kuhangaika na familia yangu kwa kipindi hiki kigumu kwetu Mungu awabariki saana kwa kazi kubwa mliofanya hapa Muhimbili yakuaga mwili wa Mwanangu na Hatimaye kijijini Kwetu Ntokela Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya alisema Award na kuongeza.

“Hatuna cha kuwalipa ndugu zangu wa Dar mliotusaidia hapa Mungu awabariki saana naomba mzidi kutuombea,Mwanangu umetangulia kwake sote tutarejea, Amina”

Awali alisema Marehemu alifikwa na mauti Machi 6, mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mfupi na kukimbizwa Muhimbili ambapo baada ya vipimo aligunduliwa kuwa na Maralia kali lakini wakati madaktari wakihangaika kumpa matibabu aliaga dunia.

Amemtaja marehemu kuwa ni Negro Award Mpandila(7) ambapo aliwashukuru Wafanyabiashara kutoka jijini Dar es salaam,Marafiki kutoka Hospitali ya Mkoa wa Mbeya na wengine wengi kupitia mitandao ya kijamii kama whatsap fb tumezidi kupata salaamu kupitia humo Bila kusahau Mysaccos ya Dar , Njombe forum, mwapima forum, makete yetu online.


Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi amina.

No comments: