Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, March 9, 2016

DK.MARY MWANJELWA AAZIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTOA MSAADA IYUNGA SEKONDARI.

Msaidizi wa Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya(CCM), Bahati Mwakatika akimkabidhi mashuka Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Iyunga kutokana na kupatwa na janga la moto ulioteketeza mabweni mawili ya shule hiyo, Msaada huo ulitolewa na Dk. Mary Mwanjelwa.

Msaidizi wa Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya(CCM), Bahati Mwakatika akiwa na wanafunzi wa shule ya  Sekondari ya Ufundi Iyunga wakipokea msaada wa mashuka na magodoro yaliyotolewa na Mbunge Dk. Mary Mwanjelwa, kutokana na kupatwa na janga la moto ulioteketeza mabweni mawili ya shule hiyo.


KATIKA maadhimisho ya kilele cha siku ya Mwanamke duniani, Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya(CCM), Dk. Mary Mwanjelwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msaada wa magodoro na mashuka katika shule ya sekondari ya Ufundi ya Iyunga iliyopo jijini Mbeya.
 
Msaada huo umekuja kufuatia mabweni mawili ya wanafunzi katika shule hiyo kuteketea kwa moto katika nyakati  tofauti na kusababisha hasara kubwa kwa shule na wanafunzi waliokuwa wakiyatumia mabweni hayo.


Akizungumza kwa niaba yake shuleni hapo jana, msaidizi wa Mbunge huyo,Tumaini Ambakisye Mwakatika, alisema Dkt.Mwanjelwa ameguswa na kusikitishwa na tukio hilo na kwamba ameamua kutoa msaada wa magodoro
na mashuka kwa wanafunzi walioathirika na tukio hilo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani.




“Mhe. Dkt. Mwanjelwa kama kiongozi mwanamke, amesikitishwa na tukio la moto katika bweni la wanafunzi lililotokea siku ya Jumatatu na ametumia siku ya maazimisho ya wanawake kuja kuwaona kwakutoa magodoro 20 na mashuka 40 na akitoka Dar es Salaam ameahidi kufika hapa shuleni kwa ajili ya kuja kuwaona” alisemaTumaini.



kwa upande wake Dk. Mary Mwanjelwa akizungumza kwa njia ya simu alisema siku ya mwaname duniani haidhimishwi kwa kutoa misaada kwa wanawake pekee bali kwa kufanya shughuli zinazoigusa jamii nzima.
 
“Maandiko matakatifu  yanasema kuwa lieni na wanaolia, hivyo licha ya kuwa mbali, nimeona nitangulize msaada huo” alisema Mbunge huyo.




“Mimi ni mama, nimeumizwa sana na tukio hili la kuungua bweni la shule ya Iyunga ambayo ni moja ya shule za kihistoria katika mkoa wetu wa
Mbeya, nashukuru Mungu nimepokea taarifa kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Mbeya ndugu Nyerembe Munasa, kuwa hakuna mwanafunzi ambaye ameathirika na moto huo” alisema mbunge huyo.

kwa upande wake  Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyerembe  Munasa, alimwambia msaidizi wa
mbunge huyo kuwa, msaada huo ni mkubwa na Dkt. Mwanjelwaanapaswakupewa sifa katika kujitoa kwake hasa kwa wahitaji na tayari tume
imeundwa kuchunguza tukio hilo ambalo lina sentensi za utata ikiwemo kuwa wiki moja lilipoungua bweni la kwanza hakukuwa na umeme shuleni hapo.



Akipokea msaada wa magodoro 20 na mashuka 40 yaliyotolewanaDkt.MaryMwanjelwa shuleni hapo, mkuu wa shule hiyo, Edward Mwantimwa,
alishukuru na kwamba kwa sasa wapo katika kipindi kigumu sana.



Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Dkt. Stephen Mwakajumilo alisema kama bodi ni kupokea msaada wa aina yeyote kote duniani,
ambapo pia aliwawashukuru waliojitokeza kutoka CCM na Chadema.
 
“Tunaomba Dkt.Mwanjelwa atusaidie kuwashawishi wengine na viongozi tutafakari pamoja kuhusu shule zote za zamani nchini hasa miundombinu ya shule hiyo”Alisema.

No comments: