Jeshi la Polisi likiondoka na Mali zinazodhaniwa kuwa za wizi |
Mali zinazosadikiwa kuwa za wizi zilizokamatwa |
Orodha ya mali iliyokamatwa |
JESHI la Polisi Mkoa Mbeya
limejikuta likitumia zaidi ya masaa manne kumtafuta mtuhumiwa wa ushirikina
bila mafanikio kutokana na mtu huyo kujigeuza Kunguru.
Tukio hilo la ajabu lilitokea juzi
kuanzia majira ya saa nne asubuhi ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kusaidiwa
na wananchi kumkamata Mwanamke mmoja aliyekuwa amejificha kiushirikina kwa
kujigeuza kunguru katika mtaa wa mapelele kata ya Ilemi jijini hapa
Tukio hilo lilitokea
baada ya polisi kufika nyumbani kwa mwanamke huyo ambaye anatuhumiwa
kumjeruhi vibaya jirani yake aitwaye Anitha Simon kwa kipigo kwa madai ya
kumuibia ndala jozi mbili aiana ya yeboyebo.
Akizungumza katika eneo la tukio,
mtoto wa kaka wa mtuhumiwa ambaye ndiye aliyefanikisha zoezi la kumkamata
,Venance Mwalindile alidai yeye ni chifu katika ukoo wao na kwamba
anakerwa na tabia za shangazi yake huyo.
“Nimeamua kufanya hivi kumuumbua
shangazi kwani nimekerwa sana na hizi tabia na ndiyo maana nimejitolea
kuwasaidia polisi mkamata ili sheria ichukue mkondo wake”alisema Mwalindile.
Hata hivyo Mwalindile alisema kuwa
ilikuwa ni kazi ngumu kwake kumkamata mama huyo anayekadiriwa kuwa na
umri wa miaka kati ya 45 hadi 50 kwani akiwa amejificha chumbani alijibadilisha
kuwa kunguru ambapo katika mapambano makali alifanikiwa kumkamata na kumnyonga
kunguru huyo ndipo aliporudi katika hali yake ya kawaida na kuwakabidhi Polisi.
Akizungumzia tukio hilo ambalo
lilijaza umati wa watu waliokuwa wakishuhudia,Mwenyekiti wa mtaa jirani wa
Mwafute Kata ya Ilemi, Charles Kasyupa alisema kuwa wamekuwa na vikao vya mara
kwa mara kuhusiana na matukio ya wizi na ugomvi wa mtuhumiwa huyo lakini
kumekuwa hakuna mwafaka.
Baada ya kufanikiwa kumkamata
mtuhumiwa huyo Polisi walifanya upekuzi katika nyumba yake na
kufaninikiwa kuvikuta vitu kadhaa vinavyodhaniwa kuwa ni vya wizi
vikiwemo Radio,magodoro,TV,madishi ya kuogea,viti vya
Kanisani,mafuta,sukari,spika za Kanisani,nguo mbalimbali na vitu vingine
ambavyo idadi na thamani yake haikuweza kufahamika mara moja.
Aidha baada ya kumaliza
kupekua nyumba hiyo majira ya saa moja jioni kwa hofu ya usalama wa wananchi
waliokuwa na hasira kali Jeshi la Polisi lililazimika kusomba mali
zilizokutwa katika Nyumba ya mtuhumiwa.
Jeshi hilo lilitumia
gari za Polisi aina ya Land cruser
zilirudia mara sita kubeba mali hiyo na kuipeleka Kituo Kikuu cha Polisi
cha Kati kwa ajili ya utambuzi wa mali hiyo wakiwa wameongozana na Mwenyekiti
wa mtaa wa Mapelele Jitihada Mwaijulu.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed
Msangi amekiri kukamatwa kwa mwanamke huyo lakini Jeshi lake bado linaendelea
na uchunguzi na atatoa ufafanuzi baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tukio
hilo
No comments:
Post a Comment