Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, March 3, 2016

DUNIA KUSHUHUDIA KUPATWA KWA MWEZI WILAYANI MBARALI MKOA WA MBEYA SEPTEMBA 1,2016


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Utalii ya UPL Gabriel Shawa akiwaonesha wanahabari mfumo wa mwendo wa jua utakaosababisha kupatwa kwa mwezi Septemba Mosi nchini Tanzania katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya


 


Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa katika kikao wakijadili namna wananchi wanavyoweza  kunufaika na Uatalii wakati wa Kupatwa kwa jua.



WAKAZI wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wametakiwa kujiandaa kupokea wageni kutoka ndani na nje ya Nchi kwa kuweka vitega uchumi mbali mbali vitakavyoweza kuwavutia watalii kwa kuweza kuinua vipato vyao.

Rai hiyo imetolewa kutokana na kuwepo kwa taarifa ya kutokea kwa tukio kubwa la kihistoria nchini ambapo Septemba mosi mwaka huu Wilaya ya Mbarali itaingia kwenye historia ya kisayansi duniani na dunia kuhamia hapo katika tukio kubwa la kupatwa kwa jua litakalotekea majira ya saa moja na nusu asubuhi siku hiyo.

Tukio hilo la kipekee duniani, linatarajiwa kuvutia wataalamu wa masuala ya unajimu kutoka sehemu mbali mbali duniani na watalii wa nje  na ndani ya nchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakifuatilia mzunguko wa mwezi na dunia.

Uchunguzi uliofanywa na Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) umebaini kuwa  baadhi ya makampuni ya utalii ya nje na ndani yameanza maandalizi kwa ajili ya tukio hilo la kipekee, ambapo  idadi kubwa ya watalii wa nje wanatarajia kuwepo mkoani Mbeya kushuhudia tukio hilo pamoja na kufurahia vivutio vingine vya utalii vilivyopo nchini.

Akizungumza wakati akichangia kwenye kikao cha Kamati ya Utalii Mkoa wa Mbeya, kilichokuwa na kazi ya kupitia mpango mkakati wa miaka mitano wa kukuza utalii katika Mikoa ya Kanda ya kusini,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kusafirisha watalii ya UPL Safaris & Tour, Gabriel Shawa alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo kamati hiyo.

Shawa aliwaeleza waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji jijini Mbeya, jana,  kuwa baada ya kubaini kuwepo kwa tukio hilo la kihistoria na nadra kutokea na kuonekana kwa uzuri zaidi kusini mwa Afrika mkoani Mbeya, wao kama watoa huduma za utalii mkoani humo  tayari wameanza maandalizi ya malazi kwa wageni wao na kuyatambua maeneo ya vivutio kwa ajili ya watalii hao.

Hata hivyo, pamoja na kuwepo kwa tukio hilo na maandalizi yake, ilibainika kuwa sio wenye hoteli wala viongozi wa serikali au wasimamizi wa sekta hiyo ya utalii waliokuwa wanaufahamu wa kuwepo kwa tukio hilo na maandalizi ya kuwapokea wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Kwa mujibu wa maelezo ya kisayansi kuhusu tukio hilo, kupatwa kwa jua hutokea pale mwezi unapopita kati ya dunia na jua hivyo kuzuia mwanga wa jua kuifikia dunia au kuifikia kwa kiwango cha mwanga hafifu.

Mtandao wa http://eclipse.astronomie.info/sofi unaonyesha kwamba tukio la kupatwa kwa jua mkoani Mbeya na hususani katika wilaya ya Mbarali litaonekana majira ya asubuhi  na wananchi wataweza kulishudia tukio hilo kwa kutumia vifaa maalumu ya kuonea kupatwa kwa jua.
  
Kanda ya Kusini ipo katika mkakati mkubwa wa kuendeleza utalii katika mikoa yake ambayo huko nyuma haikupewa nafasi ya kuwa sehemu nzuri ya utalii, japokuwa ni ukanda wenye vivutio vingi na vya aina anuai.

Katika kuviendeleza vivutio hivyo Mkoa wa Mbeya umeandaa Mpango Mkakati wa kukuza na kuendeleza utalii mkoani humo ambao utawezesha kutangaza, kukuza na kuendeleza sekta ya utalii mkoani humo nakuongeza pato la jamii na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa TAJATI,Ulimboka Mwakilili alisema kuwa timu ya waandishi hao wanaendelea kufuatilia habari za tukio hilo na kuzidi kutangaza vivutio vya utalii ili kuweza kuwavutia watalii wengi wa ndani na nje wakisukumwa na tukio hilo.


No comments: