Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, February 5, 2016

UNIDO KUWANUSURU VIJANA NA UKOSEFU WA AJIRA.


Mwezeshaji wa Program ya kunusuru vijana kutokana na ukosefu wa ajira, Dk.Omary Swalehe wa Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam akitoa maelekezo kwa wahitimu kwenye mafunzo ya awali(hawapo pichani)


Mratibu wa Taifa wa Shirika la Kimataifa la kuhudumia Viwanda, UNIDO. Deodat Bernard akitoa mada kwa Wahitimu wa Vyuo vikuu kuhusu Program ya kupambana na ajira kwa vijana

Mwezeshaji wa Programu ya ajira kwa vijana Dk.Darlene Mutalemwa kutoka Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam akieleza umuhimu wa vijana kujiunga na mpango huo.

Afisa maendeleo ya Biashara wa SIDO Mkoa wa Mbeya, Merina Mkuchu akisisitiza jambo kwa vijana waliojitokeza katika ukumbi wa Mkapa kuhusu mpango wa ajira(hawapo pichani)Baadhi ya Wahitimu wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa WawezeshajiBaadhi ya Wajisiliamali wadogo na Kati wa Jiji la Mbeya wakielezwa juu ya umuhimu wa kuwapokea Vijana waliohitmu Vyuo Vikuu katika Biashara zao ili kubadilishana nao ujuziSERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Mashirika ya kimataifa imeandaa mpango wa jinsi ya kuwasaidia vijana waliohitimu katika Vyuo vikuu ili wawe na uwezo wa kupata ajira bila kutegemea kuajiriwa.

Akizungumza katika Mafunzo kwa Vijana waliohitimu Vyuo vikuu kuanzia ngazi ya Diploma, Mratibu wa Taifa wa Shirika la kimataifa la Maendeleo ya Viwanda(UNIDO), Deodat Bernard alisema Serikali ilikuja na mpango huo ili kuona jinsi inavyoweza kutatua changamoto ya ajira kwa vijana.

Alisema katika Mpango huo ambao uliratibiwa na Shirika la UNIDO kwa kushirikiana na Shirika la Kazi(ILO),shirika la Chakula (FAO) na UN Women ambao walichagua program ya kuimarisha jinsi vijana wanavyoweza kupata ajira Program inayoendeshwa na Chuo kikuu cha Mzumbe.

Alisema katika Program hiyo vijana watakaochaguliwa wataweza kufanya kazi ya kujitolea na Wajasiliamali wa kati na wadogo ili waweze kupata ujuzi kwa vitendo pamoja na kuwasaidia wajasiliamali kuongeza na kuinua shughuli zao kupitia vijana waliosoma.

Kwa upande wao Wawezeshaji wa Programu hiyo, Dk.Omary Swalehe na Dk.Darlene Mutalemwa kutoka Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam walisema program hiyo kwa majaribio inawalenga vijana 150 nchi nzima na kwamba tayari maelekezo yamefanyika katika ya Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza na Zanzibar.

Dk. Swalehe alisema mpango huo utaanza kutekelezwa Mwezi huu February hadi Juni Mwaka huu ambapo baada ya kufanya tathmini na kubaini mafanikio kwa Wajasiliamali kunufaika ama Wahitimu kuleta tija ndipo mikakati ya kuifanya iwe endelevu itafanyika.

Alisema Mpango huo unaofadhiliwa na Kampuni ya Maendeleo la Sweden(SIDA) Wahitimu watapewa vyeti baada ya miezi mine ya majaribio ambapo watakuwa wakijitolea kwa gharama zao na kwamba vyeti hivyo vitakuwa na nembo ya Chuo kikuu Mzumbe na UNIDO ili kumuongezea sifa atakapopata nafasi ya kuitwa kazini.

Kwa  upande wake Afisa maendeleo ya Biashara wa SIDO, Merina Mkuchu mbali na kuipongeza UNIDO aliwasihi vijana watakaofuzu kwenda kuzitumia taaluma zao kwa vitendo ili kujiimarisha na kujifunza zaidi ikiwa ni pamoja na kumsaidia Mjasiliamali.

Alisema wanapoingia kwenye huo mpango wasiwe na wasiwasi na taaluma na sifa za masomo waliopitia Vyuoni bali kupitia Mjasiliamali anaweza kubadili mawazo na kuendelea na ujasiliamali ama kuajiriwa na Mjasiliamali aliyekuwa akisaidiana nae kwenye kazi.


No comments: