Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, February 5, 2016

ASASI ZA KIRAIA NA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI WA HALMASHAURI ZA MIKOA YA MBEYA, RUKWA NA KATAVI WAPASUA JIPU KWA TUME YA UCHAGUZI NEC. 
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka NEC, Hamis Mkunga aliyemwakilisha Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi  akifungua mkutano na viongozi wa Asasi za Kiraia

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya mjini ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro akielezea Changamoto alizoziona kwenye uchaguz wa Oktoba 2015

Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mbeya, Costantino Mushi akifunga mkutano wa Tume na Viongozi wa Asasi za Kiraia

Afisa Maendeleo ya Jamii Jiji la Mbeya Vicent Msola akielezea mapungufu aliyoyabaini wakati wa Uchaguzi mkuu uliopita

Washiriki wakifuatilia mada na mijadala inayoendelea


TUME ya Uchaguzi NEC imekutana na viongozi wa Asasi za Kiraia na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri za Mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi kufanya tathmini ya Uchaguzi uliofanyika Oktoba 2015.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya GR iliyopo Soweto Jijini Mbeya, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka NEC, Hamis Mkunga aliyemwakilisha Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alisema lengo la kikao hicho ni kufanya tathmini ya Uchaguzi mkuu uliopita.

Kwa upande wake washiriki wa mkutano huo walisema Uchaguzi ulijawa na changamoto nyingi ambazo Tume inapaswa kuzifanyia kazi mapema kabla ya uchaguzi mwingine kuitishwa.

Walisema Changamoto hizo ni pamoja na kuimarisha daftari la wapiga kura kuanzia sasa kwa kuwaandikisha vijana ambao kwa sasa umri umeshafika na vigezo vya kupiga kura katika uchaguzi ujao watakuwa wametimiza.

Lucy Mng’ong’o na Faustina Valleri walisema mbali na elimu kwa mpiga kura zilizotolewa na Asasi za kiraia bado kunachangamoto za wananchi kutojitokeza kupiga kura huku idadi kubwa ya wanaoharibu kura pia kuwa kubwa.

Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya mjini ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro alisema Changamoto zinazoukumba uchaguzi zinatokana na maandalizi na utekelezaji wake kuwa kama dharula.

Alisema suala la ucheleweshaji wa vifaa, kutokutimia na majina ya mpiga kura kutokuwepo kwenye daftari ili hali kitambulishi anacho bado ni changamoto inayojirudia kila uchaguzi hivyo ni vema Tume ikaziamini Halmashauri kuhakiki vifaa vyote vinavyotakiwa kabla ya kumkabidhi wakala.

No comments: