Waandishi kutoka Chama cha Waandiishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) wakifanya mahojiano na wahifadhi wa Hifadhi ya Mlima Rungwe katika lango kuu kabla ya kuingia hifadhini. |
Waandishi wakiendelea na safari ndani ya Hifadhi |
Waandishi wakipumzika katika eneo linaloitwa Kandoro Camp site iliyoko ndani ya Hifadhi ya Mlima Rungwe |
Safari ikiendelea ndani ya Hifadhi ya Mlima Rungwe |
Baada ya pumzi kukata baadhi wakalazimika kupumzika na kupata chochote ili kurudisha nguvu. |
SERIKALI imetakiwa kujenga na
kuimarisha njia yenye urefu wa kilomita nne kutoka Kijiji cha Kyimo juu katika
barabara kuu ya Mbeya Malawi kuelekea katika Hifadhi ya Mlima Rungwe katika
kijiji cha Syukula wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ili kuongeza idadi ya watalii.
Wito huo ulitolewa mwishoni mwa
wiki na Muongoza watalii katika Hifadhi ya Mlima Rungwe,Mazao Fungo alipokuwa
akizungumza na Waandishi wa Habari wa Chama cha waandishi wa habari za Utalii
na Uwekezaji Tanzani (TAJATI)waliotembelea hifadhi hiyo kwa ufadhili wa Shirika la uhifadhi mazingira(Wildlife Conservation Society)WCS).
Alisema idadi ya watalii
haiongezeki kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu inayopelekea
kushindwa kufika kirahisi katika geti lililopo katika kijiji cha Syukula.
Alisema idadi kubwa ya watalii ambao
huingilia shilingi 3000 kwa watanzania na dola kumi kwa wageni hufika watalii 200
kwa mwaka hivyo kungekuwa na miundombinu mizuri hifadhi hiyo ingekuwa na
watalii wengi zaidi.
Kwa upande wake Mhifadhi mkuu
wa Msitu wa hifadhi mazingira hai Rungwe(TFS), Innocent Lupembe alisema mbali
na kutokuwa na barabara ya kufika getini pia kutojulikana ni moja ya sababu za
kupungua kwa watalii.
Alisema Mlima Rungwe una
vivutio vingi ambavyo havipatikani popote duniani lakini havijulikani kutokana
na kutotangazwa vizuri ili kujulikana nje na ndani ya nchi ili kuongeza idadi
ya watalii.
Alisema katika mlima Rungwe
kuna Nyani adimu duniani anayepatikana katika mlima huo pekee anayejulikana kwa
jina la Kipunji ambae aligunduliwa na Shirika la Uhifadhi mazingira(WCS) mwaka
2004.
Alisema katika mlima huo
watalii wataweza kufurahia uoto wa asili uliojaa misitu iliyofunga, ukanda wa
nyasi, ukanda wa mianzi na misitu yenye uwazi, Kreta pamoja na wanyama aina
mbali mbali akiwemo Kipunji, Ngedere, Mbega, Nguruwe pori na Mbawala.
Aliongeza kuwa upo mkakati
uliyowekwa na TFS wa kujenga barabara kwa kiwango cha changarawe kwa ufadhili
wa Grobal Invaromentala facility,UNDP na WCS ili kuwapunguzia adha watalii ya
kufika katika mlima Rungwe.
No comments:
Post a Comment