Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, February 2, 2016

MIUNDOMBINU MIBOVU YAKWAMISHA WATALII HIFADHI YA MLIMA RUNGWE

 
Waandishi kutoka Chama cha Waandiishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) wakifanya mahojiano na wahifadhi wa Hifadhi ya Mlima Rungwe katika lango kuu kabla ya kuingia hifadhini.

Waandishi wakiendelea na safari ndani ya Hifadhi

Waandishi wakipumzika katika eneo linaloitwa Kandoro Camp site iliyoko ndani ya Hifadhi ya Mlima Rungwe

Safari ikiendelea ndani ya Hifadhi ya Mlima Rungwe

Baada ya pumzi kukata baadhi wakalazimika kupumzika na kupata chochote ili kurudisha nguvu.
SERIKALI imetakiwa kujenga na kuimarisha njia yenye urefu wa kilomita nne kutoka Kijiji cha Kyimo juu katika barabara kuu ya Mbeya Malawi kuelekea katika Hifadhi ya Mlima Rungwe katika kijiji cha Syukula wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ili kuongeza idadi ya watalii.
 
Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Muongoza watalii katika Hifadhi ya Mlima Rungwe,Mazao Fungo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari wa Chama cha waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzani (TAJATI)waliotembelea hifadhi hiyo kwa ufadhili wa Shirika la uhifadhi mazingira(Wildlife Conservation Society)WCS).
 
Alisema idadi ya watalii haiongezeki kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu inayopelekea kushindwa kufika kirahisi katika geti lililopo katika kijiji cha Syukula.
 
Alisema idadi kubwa ya watalii ambao huingilia shilingi 3000 kwa watanzania na dola kumi kwa wageni hufika watalii 200 kwa mwaka hivyo kungekuwa na miundombinu mizuri hifadhi hiyo ingekuwa na watalii wengi zaidi.
 
Kwa upande wake Mhifadhi mkuu wa Msitu wa hifadhi mazingira hai Rungwe(TFS), Innocent Lupembe alisema mbali na kutokuwa na barabara ya kufika getini pia kutojulikana ni moja ya sababu za kupungua kwa watalii.
 
Alisema Mlima Rungwe una vivutio vingi ambavyo havipatikani popote duniani lakini havijulikani kutokana na kutotangazwa vizuri ili kujulikana nje na ndani ya nchi ili kuongeza idadi ya watalii.
 
Alisema katika mlima Rungwe kuna Nyani adimu duniani anayepatikana katika mlima huo pekee anayejulikana kwa jina la Kipunji ambae aligunduliwa na Shirika la Uhifadhi mazingira(WCS) mwaka 2004.
 
Alisema katika mlima huo watalii wataweza kufurahia uoto wa asili uliojaa misitu iliyofunga, ukanda wa nyasi, ukanda wa mianzi na misitu yenye uwazi, Kreta pamoja na wanyama aina mbali mbali akiwemo Kipunji, Ngedere, Mbega, Nguruwe pori na Mbawala.
 
Aliongeza kuwa upo mkakati uliyowekwa na TFS wa kujenga barabara kwa kiwango cha changarawe kwa ufadhili wa Grobal Invaromentala facility,UNDP na WCS ili kuwapunguzia adha watalii ya kufika katika mlima Rungwe.
 

No comments: